Na Mwandishi
Wetu, Handeni
KAMPUNI ya
Mwananchi Communication Ltd (MCL), imejitokeza kudhamini Tamasha la Utamaduni
wilayani Handeni mkoani Tanga, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 katika
Uwanja wa Azimio Handeni Mjini na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Tamasha hilo
linalojulikana pia kwa jina la Handeni Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza
likiwa na shauku ya kutangaza utamaduni na fursa nyingine za kimaendeleo
wilayani humo, kama sera ya kuwapatia maendeleo.
Akizungumza
jana mjini hapa, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema wamekubaliana
na wenzao Mwananchi kwa ajili ya kuwezesha tamasha hilo. Alisema kitendo cha
Mwananchi kuingia katika tamasha hilo ni kuonyesha ushirikiano mkubwa waliokuwa
nao katika jamii ya Kitanzania.
“Wakati
naandaa tamasha hili sehemu mbalimbali niliweza kuingia kwa ajili ya kusaidiana
na wadau juu ya Tamasha la Handeni linalofanyika kwa mara ya kwanza, huku
likijiweka katika nafasi nzuri mno.
Tunashukuru
kwa wale walioguswa na kujitokeza kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa
Kampuni kama Mwananchi kuingia ni cha kuungwa mkono na Watanzania wote kwa
ajili ya kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa mazuri,” alisema Mbwana.
Kuelekea kwa
tamasha hilo, vikundi mbambali vimeonyesha kuliunga mkono tamasha hilo
litakalowaunganisha Watanzania wote, hususan wakazi wa wilaya ya Handeni,
mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla.
Wadhamini wengine ni Phed Trans,
Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa
Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN
B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD)
na Michuzi Media Group duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind
& Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha
‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa
Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi saa 12 za jioni.
No comments:
Post a Comment