October 26, 2013

FAMILIA YA TSN YAENDELEA KUPATA WASOMI

FAMILIA ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (Tanzania Standard News Papers (TSN) Limited) imeendelea kupata wasomi katika nyanja mbalimbali. Pichani ni Wahitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii na Uongozi kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Theipista Nzanzugwanko ambaye ni Mwandishi wa gazeti la HABARILEO (kulia) akiwa na Albina Kivae, Msanifu Kurasa wa TSN idara ya Matangazo wakiwa na furaha baada ya kutunukiwa nondo zao hii leo katika mahafali ya 25 ya Chuo hicho huko Kibaha mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment