Lakini ndani ya mioyo yao, mamilioni ya watu wanaompenda wanajua vyema kuwa jambo hilo haliwezi kuepukika.
Mandela amekuwa akiugua mara kwa
mara katika siku za hapo nyuma, raia wa Afrika Kusini ndio sasa wanaanza
kuona dalili na kukubali kuwa Mandela naye ni binadamu kama watu
wnegine popte duniani.
Hata hivyo mada hii bado ni jambo ambalo haliwezi kuzungumziwa hadharani nchini Afrika Kusinui.
Somadoda Fikeni, mkuu wa shirika la hifadhi za
Afrika Kusini, anasema hatuna mtu tunayeweza kumfananisha na Mandela
hapa Afrika Kusini na kote duniani.
"watu wanamuona kama tiba kwa maradhi yaliyo
katika jamii au maovu yanayotokea katika jamii . Na ndio maana watu
hawataki kukubali kuwa Mandela atawaaacha hata siku moja. ''
Kulingana na utamaduni wa Afrika Kusini, wale walio wagonjwa sana hawafi hadi familia 'inapowaachilia' kiroho
Raia wa Afrika Kusini wanamuona Mandela kama
gundi ambayo inashikilia jamii pamoja na wanaamini kuwa mabadiliko
katika jamii, umaskini, ufisadi na ukosefu wa ajira yanaweza kuangamizwa
ikiwa tu Mandela atasalia kuwapa muongozo viongozi wa wengine nchini
humo.
Hii inaweza kuwa ni ndoto kubwa kumwekea mtu mmoja , lakini machoni mwa wengi, Mandela sio binadamu wa kawaida.
Hata hivyo, kwa mara ya kwanza inaonekana kuwa
kilio kinachomzingira Mandela anapougua mara kwa mara kinaanza
kubadilika kwa sauti.
Jarida la Sunday Times mwishoni mwa wiki, lilikuwa na kichwa: Ni wakati kumruhusu aende zake.''
Ni kauli ambayo inazua hisia kwa familia ya Mandela na watu wengi Afrika Kusini.
Kawaida wito ambao hujitokeza hasa afya ya Mandela inapoendelea kuzorota ni watu wamuombee.
Lakini haya hayakuwa maneno ya mtu wa kawaida
kuhusu sura anayotoa Mandela kwa jamii.Yalikuwa maneno ya rafiki yake na
mfungwa mwenzake katika gereza la Roben Island, Andrew Mlangeni, baada
ya kupokea habari kuwa Mandela amelazwa tena hospitalini.
"familia yake lazima imwache aende zake, ili
Mungu afanya atakalo naye...Pindi familia itakapofanya hivyo, nao watu
wa Afrika Kusini wataweza kumruhusu aende zake,'' alinukuliwa akisema
bwana Mlangeni.
Wengi wanafahamu fika kuwa hali mbaya ya kiafya ya Mzee Mandela, inaendelea kuzorota, lakini kwa hali hiyo hiyo wanamtaka aweze kuishi maisha marefu.
Ni uhusiano wa kipee walio nao Mandela.
''Huenda ikawa mzozo katika familia yake ndiyo
inampa wasiwasi na hilo linahitajika kusuluhishwa wakati akiwa bado hai.
Huenda asipokelewe vyema, upande huo wa pili hadi mambo haya
yatakaposuluhishwa,'' alisema Mlangeni
Mtu yeyote ambaye amewahi kumpenda baba au babu
yake anaweza kushuhudia kuwa yeye kawaida hataki mtu yule
kuondoka...watu nchini Afrika Kusini wanamuona Mandela kama baba yao
asiyekuwa na kifani.
Mandela alizuia kutokea kwa vita vya wenyewe kwa
wenyewe, alipotoa wito wa waafrika weusi na wazungu kuungana pamoja na
kusameheana baada ya vita alivyoongoza dhidi ya ubaguzi wa rangi, wakati
ambapo Afrika Kusini kama nchi ilionekana karibu kuporomoka.
Lakini nchi hiyo ingali inakabiliwa na
mgawanyiko, ubaguzi wa rangi kujitokeza mara kwa mara na chama wa ANC
kimegawanyika kuliko wakati wowote ule.
Mandela alichiliwa baada ya miaka 27 gerezani kufuatia vita vyake dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Ukabila unaanza kujitokeza nchini humo, baadhi ya wataalamu wanasema kuwa hii ni kutokana na kukosekana kwa uongozi thabiti.
Migawanyiko hii inawalazimisha raia wa Afrika
Kusini kuitizama upya ndoto ya Nelson Mandela ya nchi ya mshikamano
licha ya rangi ya watu na ikiwa ndoto hiyo itawahi kutimizwa.
Baadhi wangali wanaamini kuwa Afrika Kusini inaweza kujikwamua na kujipa hadhi ya juu zadi kama iliyokuwa ndoto ya Mandela. SOURCE: BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment