Mwenyekiti
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akijadiliana jambo na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi
Kusini Mwa Afrika SADC Dkt.Tomaz Salomao mjini Cape Town Afrika ya
Kusini leo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(Watatu kushoto) akiongoza kikao maalum cha
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC kilichofanyika jijini Cape Town
Afrika ya Kusini leo.Wengine katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo
akiwemo mwenyeji Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(kulia),Waziri wa
Mambo ya nchi za nje wa Namibia Bibi Netumbo Nandi-Ndaitwa(kushoto) na
wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya
Kusini wakitoka katika ukumbi wa hoteli ya Westin jijini Cape Town
Afrika ya Kusini mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati ya
Ulinzi na Usalma ya SADc kilichofanyika leo.Rais Kikwete alikuwa nchini
Afrika ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mkurugenzi Mtendaji na mratibu
wa asasi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bwana Mark Suzman jijini
Cape Town Afrika ya Kusini.Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Adam Malima.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagana na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la
Misaada la Marekani USAID Dkt. Rajiv Shah muda mfupi baada ya kufanya
naye mazungumzo katika ukumbi wa Cape Town Convention Centre jana.
No comments:
Post a Comment