Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano cha Barclays Tanzania, Bibi Tunu Kavishe, (shoto),akizungumza na Wanahabari mapema leo ndani ya hotel ya Serena Jijini Dar,kuhusiana na Benki ya Barclays kuaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step Ahead Walk,Mchakato ambao umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006,ambapo pia Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.
Matembezi
hayo ya hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu wa
benki ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia
mahitaji muhimu katika jamii. Tangu ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati
huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha uchangishaji fedha ili kusaidia
masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga– ambayo ni muhimu kwa jamii
yetu.
Msanii
wa Muziki wa kizazi kipya Barnaba Elias akizungumzia wimbo wake
alioutunga na Mwanamuziki mwenzake Jean Pierre ajulikanae kwa jina la
Kidumu ambao umezinduliwa leo rasmi ukiitwa ‘Wanawake”,"Wimbo huo umetungwa na kuimbwa na Barnaba Elias anaejulikana kama ‘Barnaba’
na Jean Pierre Nimbona anaejulikana kama ‘Kidumu’ ambao lengo lake na
maudhui ni kuhamasisha watu wote wakazi wa Tanzania wajitokeze katika
kuchangia na kuhudhuria matembezi haya ya hisani ambayo lengo lake rasmi
ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama na watoto wachjanga"alisema
Barnaba.
*************
Kila
mwaka Benki ya Barclays inaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa
kwa jina la Step Ahead Walk. Mchakato huu umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006 na
Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia
matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.
Matembezi
haya ya hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu wa benki
ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji
muhimu katika jamii. Tangu
ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha
uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga–
ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.
Akiongea
katika vyombo vya habari leo, Bibi Tunu Kavishe, Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano na Mahusiano cha Barclays Tanzania amesema, leo hii tunazindua
mziki unaoitwa ‘Wanawake” ambao umetungwa na kuimbwa na Barnaba Elias
anaejulikana kama ‘Barnaba’ na Jean
Pierre Nimbona anaejulikana kama ‘Kidumu’ ambao lengo lake na maudhui ni
kuhamasisha watu wote wakazi wa Tanzania wajitokeze katika kuchangia na
kuhudhuria matembezi haya ya hisani ambayo lengo lake rasmi ni kuchangisha pesa
kwa ajili ya kinamama na watoto wachjanga.
Tukio hili rasmi itafanyika tarehe 8
juni, 2013 katika hoteli ya Golden Tulip na litahusisha matemebzi ya hisani ya
kilomita tano (5) na kila mtu katika jamii anakaribishwa kushiriki. Tiketi zitauzwa
kwa shilingi za kitanzania 5000 na zitapatika katika kila tawi la Benki ya
Barclays kuanzia tarehe 29 Aprili, 2013.
Mwaka
2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kuchangisha shilingi za
kitanzania milioni 150 kutokana na mauzo
ya tiketi na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili. Mwaka huu lengo ni
kuchangisha zaidi ya marambili ya shilingi milioni 150 kutoka kwenye matoleo ya
washirika muhimu na washiriki wengine katika jamii.
Fedha zitakazochangishwa mwaka huu zitakwenda kusaidia katika masuala ya uzazi na afya ya watoto kama ifuatavyo:-
1. Mafunzo kwa wakunga wa uzazi
2. Matibabu ya Fistula
3.Upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu unaosababishwa na uzazi.
Step
Ahead Walk 2013 itaweza kufanikiwa tu kama itawezeshwa na kila mshiriki na
jamii nzima ya kitanzania kwa ujumla. Kwa sababu hiyo basi tujiunge wote ili
tuweze kufanya badiliko katika masuala ya afya kwa ujumla hapa Tanzania
hususani masuala ya uzazi na afya ya watoto.
No comments:
Post a Comment