Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akiongea na
wandishi wa habari (hapo pichani) wakati wa droo kubwa ya mwisho ya
kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea
ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka
mshindi wa promosheni hiyo. Kushoto ni mshindi wa million 15 wa
promosheni ya Amka milionea bwana Juma Ibrahim Hiza mkazi wa Dar es
Saalam na kulia ni mshindi mwingine wa shilingi milioni 15 Bwana Adnan
Ayub Khan mfanyabiashara Simiyu.
****** ******
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya
promosheni ya Amka millionea na kumzawadia mshindi wa droo hiyo kitita
cha shilingi million 50.
Droo
hiyo kubwa na ya mwisho ilifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco
na kushuhudia na waandishi wa habari ambapo mkazi wa Kariakoo Dar es
Salaam Bwana Layakal Akbar Thawer mwenye umri wa 60 mafanyabiashara
wa duka la rangi aliibuka kuwa mshindi wa millioni 50 na kutangazwa
rasmi kuwa mshindi.
Akiongea
wakati wa droo hiyo, Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi
alisema, Mpaka sasa Airtel kwa kupitia promosheni ya Amka millionea
imewazawadia watanzania na wateja wengi nchini. leo tunashuhudia bwana
Akbar akiibuka kuwa mshindi wa pesa taslimu shilingi million 50 kupitia
promosheni hii ya Amka millionea na Airtel.
Hii
inathibitisha thamira yetu ya kutuoa huduma bora na bei nafuu huku
tukiendelea kuwazawadia watanzania na wateja wetu kwa kupitia promosheni
mbalimbali ikiwemo hii ya Amka millionea Tunaahiidi
kuendelea kuboresha huduma zetu na kuhakikisha tunawafikia watanzania
wengi zaidi, mpaka sasa kwa kupitia huduma ya Airtel yatosha wengi
wamepata unafuu wa gharama za mawasiliano na kuwezeshwa kupiga simu
kwenda mitandao yote nchini na kushuhudia kuwa kweli Airtel yatosha.
Tunaamini
kwa kuendelea kuongeza ubunifu katika huduma zetu na kuwazawadia
wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali pamoja na huduma bora
zikiwemo za kibenki kupitia Airtel money na huduma ya internet ya kasi
zaidi ya 3.75G wateja wataendelea kupata suluhusho la mawasiliano na za
kimtandao zilizo bora , za uhakika na gharama nafuu aliongeza Nyakundi.
Akiongea
kwa njia ya simu mshindi wa shilling million 50 bwana Layakal Akbar
Thawer alisema “ mimi nimekuwa mteja wa Airtel kwa miaka 7 sasa na
nafurahia huduma zao, napenda kuwambia watanzania washiriki promosheni
hizi nao wananafasi ya kuibuka washindi.
Promosheni
ya Amka milionea ilizinduliwa rasmi mwenzi December mwaka jana na
kuongezewa muda wake mwenzi machi mwaka huu, mpaka sasa wateja zaidi
ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi million 626
zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali
nchini.
Mshindi
mwingine wa shilingi million 50 alipatikana na kuzawadia mwenzi watatu
naye ni Mwalimu wa shule ya msingi na mkazi wa manyara kiteto bwana
Grayson Safieli Kabora , huku washindi wa shilingi million 15 wakiwa ni
pamoja na Juma Ibrahim Hamza umri wa miaka 30 na mkazi wa kawe Dar es
Saalam na Adrian Ayub khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara Simiyu
No comments:
Post a Comment