Katika hali ambayo si yakufumbuwa macho na
Serikali kupitia Wizara ya Afya ni juu ya uuzwaji wa vyandarua (NET) za
kujikinga na Mbu waambukizao ugonjwa wa Malaria ambazo ni za msaada.
Vyandarua hivyo vya Olyset Net ambazo ni maalum
kwaajili ya kugaiwa bure kwa watu waliokatika uhitaji hasa wakina mama
wajawazito sasa vinauzwa mitaani na serikali inatakiwa kufanya msako wa kubaini
wafanya biashara wanaouza vyandarua hivyo kinyume cha sheria.
Olyset Net ni vyandarua vya msaada kutoka UKaid,
Wizara ya Afya ya Kenya na Shirika la PSI Kenya na katika mifuko yake
imeandikwa FREE NET na maneno mengine ya NOT FOR SALE na UUZWAJI HAURUHUSIWI.
Lakini ili kuhalalisha uuzwaji huo wauzaji hao
ambao wanaibia wananchi wameamua kukata maeneo yote yaliyo na maneno hayo na
pindi mteja akifika huuziwa kwa Tsh 6,500/= bila punguzo la aina yeyote.
Maeneo zinapouzwa sana Vyandarua hivyo ni katika
magari madogo yanayosimama katika vituo daladala na mikusanyiko mikubwa ya watu
nyakati za jioni.
Uchunguzi wa Father Kidevu Blog umethibitisha
kuwapo kwa biashara hiyo katika maeneo ya Ubungo, Buguruni, Gongo la Mboto na
maeneo mengine kama Mbagala na Mwenge jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wameitaka Serikali kuwakamata
mara moja wauzaji hao wa vyandarua hivyo vinavyopaswa kugaiwa katika maduka ya
HATI PUNGUZO lakini kutokana na biashara hiyo vimekuwa havipatikani katika
maduka hayo.
Maneno ya NOT FOR SALE yakiwa yamekatwa katwa ili kuwababaisha wananchi kuwa si za kugaiwa bure.
Mfuko wa kuhifadhia Net hiyo ya msaada.
No comments:
Post a Comment