baadhi
ya wanafunzi wakifanya mafunzo ya ukocha kwa vitendo yaliokuwa
yakiendeshwa na kituo cha International Insparation kanda ya kaskazini
kwenye viwanja vya sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
picha
ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo yao wakiwa na nyuso za furaha baada
ya kutunukiwa vyeti na katibu wa baraza la michezo la taifa Henry
Lihaya kwenye uwanja wa Seikh Amri kalita Abeid.
******
Na Mahmoud
Ahmad Arusha
Mafunzo
ya michezo shirikishi kwa jamii ya kukuza vipaji na michezo yaliokuwa
yakindeshwa na kituo cha kuendeleza vipaji na michezo cha International
Insparation kanda ya kaskazini kwa wiki moja na kuwashirikisha zaidi ya
walimu na wanafunzi 70 yamefungwa jana jijini hapa na katibu wa BMT.
Akifunga
mafunzo hayo katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa Henry Lihaya
aliwataka wanafunzi hao kujituma na kujijenga kwenye masuala ya
kimichezo kwani kwa sasa michezo ni ajira tosha.
Huku
akiwataka kuyatumia vizuri mafunzo hayo kwa manufaa ya taifa na kujenga
miili yao sanjari na kupiga vita maambukizi ya magonjwa ya ukimwi na
Malaria kupitia michezo watakayoenda kufundisha.
“Ndugu
zangu vijana mkumbuke hivi sasa michezo ni ajira na mafunzo mtakayopata
yatawajengea uwezo na msikae nayo muende mkafundishe kama
mlivyofundishwa ilikupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na maradhi
muwe mabalozi wazuri huko muendako”alisema Lihaya
Nae
Mratibu wa Internation Inspiration mkoa wa arusha ambao wameratibu
Mafunzo hayo Samwel Mpenzu alisema kuwa mafunzo hayo yaliwashirikisha
zaidi ya walimu30 na wanafunzi 30 kutoka halmashauri ya jiji la Arusha
na yalihusu kozi ya ukocha wa michezo mbali mbali ikiwa ni muendelezo wa
kusogeza michezo kwa vijana.
Mpenzu
alisema kuwa Ujumbe wa mafunzo hao ulikuwa ni michezo kwa Afya na kuwa
mbali na mafunzo ya ukocha pia waliwafunza kujikinga na maambukizi ya
maradhi wakiwa michezoni sanjari na ushirikishi wa jamii katika kukuza
michezo hapa nchini.
“Unajua
kuwa michezo ni huduma muhimu hivyo yatupasa kuwasogezea jamii kupenda
michezo katika kupiga vita maradhi mbali mbali yanayoiandama
jamii”alisema Mpenzu.
Aidha
mwalimu wa mchezo wa riadha Francis John alisema kuwa katika mchezo huo
alikuwa na wanafunzi zaidi ya 21 na walijifunza jinsi ya kutupa
mitupo,Miruko,na Mbio na wote walifanikiwa kumaliza mafunzo hayo.
Mwanafunzi
wa shule ya sekondari Felex Mrema Greygory John 15 alisema kuwa pamoja
na kupata mafunzo hayo atayatumia vizuri kataka kuendeleza michezo hapa
jiji na mkoani huku akiwataka vijana wenzake kuacha kutumia madawa ya
kulevya kwani ni hatari kwa afya zao na huharibu maisha.
No comments:
Post a Comment