April 16, 2013

UTT YAZINDUA HUDUMA MPYA YA MIKOPO KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji  (UTT), Dk. Hamis Kibola akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kukopesha kwa ajili ya kuendeleza biashara kwa wafanyabishara wadogo na wa kati kwa masharti nafuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano, Daudi Mbaga na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.

Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akimkabidhi mkopo wa shis milioni 4 Mkuu wa madereva wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, Mrisho Ngongo.
Picha ya pamoja
Na Mwandishi Wetu
 MFUKO wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) imeanzisha huduma mpya ya kukopesha kwa ajili ya kuendeleza biashara kwa wafanyabishara wadogo na wakati kwa masharti nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mwendeshaji Mfuko huo James Washima alisema kuwa mfuko umetimiza miaka 10 ambapo imeanzisha huduma hiyo ili kuweza kukuza uchumi kwa wananchi.
Washima alisema kuwa waliowekeza katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja na UTT watachukua mikopo kwa kutumia vipande wanavyomiliki kama sehemu ya dhamana na ikiwa pamoja kuondolewa kwa gharama za kujiunga.
vipande katika mfuko huo kutarahisha kukopa na kupunguza gharama kuweza kujiunga katika uwezeshwaji wa mikopo.
Alisema kuwa waliowekeza vipande hawataweza kukopa dhamani yote iliyowekezwa katika mfuko lengo ni kuendelea kustawisha kiuchumi kwa wananchi na kuona umhimu wa uwekezaji katika mfuko huo.
Washima alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kutoa suluhisho kwa wajasiriamali wadogo ,mfuko wa kuweka na kukopa (SACCOS) na mwananchi mmoja moja katika upatikanaji wa mitaji kwa  kuwezesha kutekeleza miradi ya kiuchumi.
Aidha alisema kuwa wameweka mfumo ambao utaweza kurahisisha kuwafikia wananchi wa vijijini kuweza kukopa hata kama hawako katika mfumo wa uwekezaji wa vipande.
Alisema mikopo hiyo katika madaraja  manne ya mtu mmoja moja,kupewa dhamana ya mtu aliyewekeza katika mfuko huo,mkopo kwa ajili ya taasisi  pamoja na mkopo wa biashara.

No comments:

Post a Comment