April 25, 2013

‘ROOM TO READ’ SHIRIKA LINALOSAIDIA KUBORESHA NA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU TANZANIA

Moja ya madarasa katika Shule ya Msingi Dihinda iliyopo kata ya Mvomero ambalo limejengwa na Shirika la Room to Read.

Room to Read ni Shirika la Kimataifa lisilo la kibiashara linalojishughulisha na kuboresha na kuinua elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa na maktaba pamoja na kusambaza vitabu vya kujisomea wanafunzi sambamba na kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa kuwasaidia wanafunzi wa kike waliopata masomo na kuwainua kitaaluma katika nchi kadhaa duniani.

Kwa sasa shirika hili limefungua tawi hapa nchini Tanzania likiwa na program kadhaa za kusaidia kuboresha na kuinua kiwango cha elimu katika shule za msingi.

Mo blog ilipata fursa ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo nchini Tanzania, ambaye alitoa maelezo ya kina kuanzia historia ya shirika hilo, kuanza kwa shughuli zake hapa nchini, mafanikio yaliyopatikana na hatimaye mikakati ya shirika hilo katika siku za usoni.


Theodory Mwalongo ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room To Read ambalo ni Shirika la Kimataifa lenye Makao yake makuu huko San Francisco nchini Marekani ambako lilianzishwa mwaka 2000.
Baadhi ya Wanafunzi wilayani Mvvomero wakijisomea katika moja ya Maktaba iliyojengwa na Shirika la Room to Read Tanzania.

Akizungumzia shirika hilo Theodory Mwalongo anasimulia…………………!!
Lilianzia huko nchini Nepal na mwanzilishi wake alikuwa anaitwa John Wood ambaye alikuwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Microsoft na katika shughuli zake aliweza kupita Nepal akaona mahitaji makubwa ya watoto ya vitabu.

Akaamua kuacha kazi yake ya kutangaza biashara ya kompyuta huko Asia akaamua kurudi Marekani akawa anakusanya vitabu na kuvipeleka Nepal, lakini alipopeleka vitabu vile ikawa hakuna mahali pa kuviweka kwa sababu hakukuwa na madarasa hali ilikuwa ni mbaya sana.

Basi akaanzisha wazo la kujenga kwanza madarasa, kujenga vyumba vya maktaba na baadae kupeleka vitabu.

Basi hatimaye shirika limeena katika nchi nyingi ambapo kwa sasa Room To Read inafanya kazi zake katika nchi 10 duniani na kwa hapa Afrika ipo katika nchi 3 ambazo ni Afrika Kusini, Zambia na Tanzania.

Hapa Tanzania shirika limepata usajili wake mwezi wa 9 mwaka 2010 lakini rasmi limeanza shughuli zake mwaka 2011 kwa kazi za kuboresha elimu ya msingi.

Shirika lina programs nne (4); ya kwanza ni kuboresha miundo mbinu ya shule tukimaanisha ujenzi au ukarabati wa vyumba vya madarasa, kuwawezesha watoto kupata mahali pazuri pa kujifunzia lakini waalimu pia mahali pazuri pa kufundishia. TAARIFA ZAIDI BOFA HAPA>>>MO BLOG

No comments:

Post a Comment