Jumatano
iliyopita kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalionesha ni jinsi gani
utulivu unavyosaidia katika mashindano ambapo timu kutoka Kenya ilifanikiwa
kuzitoa timu nyingine za Tanzania, Uganda na timu nyingine kutoka Kenya .
Kenneth Kamau na Wills Ogutu walishinda katika mikwaju ya penati na kufikia
hatua ya mwisho katika ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walifanikiwa kulenga
matundu manne na kupata fedha za kimarekani dola 5,500. Kwa bahati mbaya
walishindwa kulenga tundu la mwisho na hivyo kupelekea kupoteza dola 2,500 na
kuondoka na fedha za kimarekani taslimu dola 3,000.
Kenneth
na Wills wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya
Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Katika kipindi kijacho cha
mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV,
timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kutambulika kama wachezaji na si tu
mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya
Pan-African.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa
ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika
televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi
kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15)
usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku
.
Katika
Episodi ya nne ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV
na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi
itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote
yatapatikana Jumatano hii.
Hizi
ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha nne wiki hii cha GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.
Timu
ya blu-Tanzania:
·
Lukwesa Kanakamfunu(18) na
Hamza Ziada(20), wote kutoka Dar-es-Salaam wanaojivunia kuwa marafiki japokuwa
wanashabikia timu mbili adui yaani Arsenal na Manchester United. Lukwesa ni
mwanafunzi na ndiye kichwa cha timu wakati Hamza ndiye atakayekua akionesha
uwezo wa kuchezea mpira.
Timu nyekunndu:
·
Ephatus Nyambura(24) na
Samuel Papa(23) wote kutoka Nairobi watashiriki kuona kama wanaweza kuwa timu
ya tatu ya Kenya kupata nafasi ya kufuzu mashindano ya Pan Africa. Empantus
meneja wa ujenzi na ndiye kichwa cha timu wakati Samuel ambaye ni mchezaji wa
Nakuru Allstars FC ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira.
Timu
ya kijani-Uganda:
·
Andrew Mpanga(30) na
Gadafi Mohammed Anguzu(18) wote kutoka Kampala,Andrew ni mshabiki wa Man.Utd
wakati Gadafi ni mshabiki wa Man.City.Andrew ni daktari wa meno ambaye atakuwa
kichwa cha timu.Gadafi ni mchezaji mpira hivyo ataonesha uchezaji wake.
Timu nyeusi-Uganda:
·
Badi Arorwa(25) na Dennis
Bogere(30)kutoka Kampala watawakilisha Uganda katika kipindi kijacho cha
mashindano.Badii atajibu maswali akiwa kama kichwa cha timu na Dennis ambaye
atakayekuwa akichezea mpira kuonesha kipaji chake.
Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa
kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.
Pia
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya,
Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari
zote zinazohusu mchezo huu.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya
kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia
na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya
bia uipendayo ya Guiness wakati
unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa
walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.
Tafadhali Kunywa kistarabu.
No comments:
Post a Comment