Msemaji
mkuu wa hafla ya "Marketer's Night Out " Dkt.Wale Akinyemi kutoka
nchini Nigeria akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo
pichani) waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa chini
ya udhamini mkubwa wa kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake
cha Tusker Lite.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon
akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla hiyo ya "Marketer's Night Out " ndani hotel ya Golden Tulip usiku huu jijini Dar.
Mkurugenzi
Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Ephrahim Mafuru akizungmza
mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya Usiku wa
maafisa masoko (Marketer's Night Out),uliofanyika ndani ya hoteli Golden Tulip,Masaki jijin Dar.Usiku huo umedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kipitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
Mmoja
wa watangazaji mahiri kutoka kituo cha redio, Eastafrica Radio
atambulikae haswa kwa jina la Zembwela akijitambulisha mbele ya hafla
maalum ya Usiku wa Maafisa Masoko kutoka makampuni mbalimbali,ndani ya
Golden Tulip,Masaki jijin Dar.
Pichani
shoto ni Meneja Masoko wa Multchoice-Tanzania, Furaha Samalu akiwa na
msemaji mkuu wa hafla ya Marketer's Night Out,Dkt.Wale Akinyemi kutoka
nchini Nigeria.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon akibadilishana mawazo na Mkurugenzi
wa Masoko,Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Ephrahim Mafuru kwenye
hafla ya Usiku wa maafisa Masoko kutoka kampuni mbalimbali.
Pichani kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Tusker Lite,Anitha Msangi akiwa na mdogo wake wakifurahia jambo.
Mmoja wa waimbaji mahiri ndani ya bendi ya B Band,akiimba kwa hisia kwenye hafla ya Usiku wa Maafisa Masoko
(Marketer's Night Out),iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar.
Baadhi
ya Wanamuziki wa bendi ya B Band inayoongozwa na Banana Zorro
wakitumbuiza usiku huu wenye hafla fupi ya Usiku wa Maafisa Masoko
(Marketer's Night Out),iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano
wa hotel ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar.Usiku huo umedhaminiwa na
kampuni ya bia ya Serengeti kipitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo usiku
wa leo wakimsikiliza msemaji mkuu wa hafla hiyo Dkt.Wale Akinyemi kutoka
nchini Nigeria.
No comments:
Post a Comment