Afisa
Tawala wa Mkoa wa Arusha, Jackson Saitabahu, akizindua mashindano ya mchezo wa
Darts kusaka Bingwa wa Safari Lager Afrika Mashariki na kati , jana katika
ukumbi wa Appex, kijenge, jijini Arusha.
****** ******
MABINGWA
watetezi wa kombe la Safari Lager Afrika mashariki na kati katika mchezo wa
“Vishale” Darts, Kenya wameanza vema kampeni ya kutetea ubingwa wao kwa kuibuka
wababe katika mchezo wa kwanza uliohusisha timu za Taifa (Interstate), kwa
kuifunga Tanzania kabla ya kuwatandika vibonde Uganda.
Katika
mchezo huo nafasi ya pili imeenda kwa kikosi cha Tanzania One, huku ndugu zao
Tanzania Warriors wakijituliza katika nafasi ya tatu na kuwachapa Uganda kwa
tofauti ya pointi Tatu.
Awali
akizindua mashindano hayo ya siku tatu, Afisa Tawala wa Mkoa wa Arusha, Jackson
Saitabahu amesema kuwa, Lengo la mashindano yawe ni kuboresha muungano wa
jumuiya ya Afrika mashariki na kuongeza mshikamano wa kimichezo miongoni mwa
nchi wananchama.
Kwa
upande wake Raisi wa Shirikisho la mchezo wa Darts Taifa (TADA) na Afrika
mashariki, Gesasu Waigama amesema kuwa kutoka na ushiriki wa mwaka huu
TADA na Jumuiya nzima inatarajia kuona mchezo huo ambao kwa siku za hivi
karibuni umekuwa ukipoteza umaarufu utarudia hali yake ya zamani.
Akizungumzia
baadhi ya changamoto zinazokabili mchezo huo, Katibu mkuu wa Darts Taifa, Kaale
Mgonja amesema kuwa mchezohuo umekosa hamasa kutokana na kuchezwa katika kumbi
za starehe sehemu ambazo watu wengi sio rahisi kufika na kuitaka serikali kutoa
mchango wake katika mchezo huo.
Mashindano
ya Darts Afrika Mashariki 2013 yanadhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia kinywaji cha Safari Lager ambapo zaidi ya wachezaji 200 wanashiriki
kutoka katika nchi za Kenya, Uganda na mwenyeji Tanzania.
Katika
mashindano kuna michezo ya wachezaji mmoja mmoja (singles and doubles), michezo
ya kitimu (team games), pamoja na ile ya jumuiya iliyopigwa katika siku
ya ufunguzi.
No comments:
Post a Comment