April 17, 2013

BI KIDUDE AFARIKI DUNIA


Nguli wa Muziki wa Mwambao nchini na barani Afrika Fatuma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude (zaidi ya miaka 90) amefariki mchana huu.



Taarifa zilizoifikia Father Kidevu Blog zinasema kuwa Bi Kidede amefariki majira ya saa 7 mchana wa leo nyumbani kwa ndugu yake huku Bububu Kisiwani Zanzibar.



Aidha taarifa hizo zinaelezo kuwa Mipango yua kuusafirisha mwili wa Marehemu inafanyika kutoka huko Bububu hadi Nyumbani kwake Raha Leo.



Bi Kidude aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa na kulazwa mara kadhaa kifo chake kinaelezwa pia kuchangiwa zaidi na umri mkubwa.



Msiba huu ni mzto kuwahi kutokea kwa tasnia ya muziki na Sanaa kwa ujumla kufuatia Mchango mkubwa wa Marehemu katika kukuza muziki halisia wa mwambao.



Rais Jakaya Kikwete alimtunuku Bi Kidude Nishani ya Uhuru wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika kipindi cha uhai wake.


Father Kidevu Blog inaungana na watanzania wote na wapenzi wa burudani ulimwenguni kwa msiba huu na itatoa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment