Mkuu wa Usambazaji
Musa Kito akiwa ameshikilia Sanduku la Dhahabu, wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni
ya Maisha Bomba na Baclays ndani ya Sanduku kla Zahabu uliofanyika leo katika
Ofisi za beki hiyo tawi la Morocco jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa kitengo
cha biashara cha benki ya Barclays Tanzania, Samuel Mkuyu (kulia) akiwa pamoja
na Meneja Masoko wa Baclays, Rahma Ngassa (kushoto), Mkuu wa Usambazaji Musa
Kito na Afisa Mawasiliano, Lilian Machera wakiwa wameshikilia Sanduku la
Dhahabu, wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Maisha Bomba na Baclays ndani
ya Sanduku kla Zahabu uliofanyika leo katika Ofisi za beki hiyo tawi la
Morocco jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Baclays Bank tawi la Morocco jijini Dar es Salaam wakiwa katika uzinduzi huo.
******** **********
Barclays Tanzania leo imetangaza rasmi
uzinduzi wa kampeni yake ya Sanduku la Dhahabu kwa wateja wake muhimu wa sasa
na wale wanaolengwa kwa baadaye.
Barclays itaendesha
kampeni hii muhimu ambayo itawapa wateja wao muhimu fursa ya kujishindia zawadi
mbalimbali kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3). Ukiweka pesa zako benki na
ukaweza kubakisha salio lililokusudiwa, wewe ukiwa kama
mteja wetu wa sasa na hata yule mpya utaweza kuingia kwenye droo ambapo wateja
10 watajinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia zawadi ya
shilingi millioni kumi za kitanzania (Tsh 10,000,000). Promosheni hii inaanza leo hii tarehe 11 Aprili
2013 hadi tarehe 30 Juni 2013 (3)
Akiongea na waandishi wa habari leo hii, Kaimu Mkuu
wa kitengo cha biashara cha benki ya Barclays Tanzania bwana, Samuel Mkuyu amesemashindano hili liko wazi kwa wale wateja wapya na wa zamani wenye akaunti za binafsi ambao wanahifadhi pesa zao na benki yetu
hapa tanzania kwenye akaunti ya Kuweka”.
Akiongezea wateja ambao watatakiwa kuingia katika
promosheni hii ni wale tu wenye akaunti za Hundi na Akiba, na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye akaunti mpaka
lifikie shilingi laki tano za kitanzania (Tsh 500,000), na salio hili libakie
kwenye akaunti bila kupungua ndani ya mwezi wa shindano.
Kwa wale wateja wapya wanaweza wakaweka shilingi laki tano kwenye akaunti
zao bila kuzipunguza na wakaingia kwenye shindano la mwezi walioweka pesa zao. Wateja
wetu wote wa sasa na wapya wataweza kuingia na kujishindia zaidi ya mara moja
iwapo wataongeza ziada ya shilingi laki tano (Tsh.500,000 ) ndani ya mwezi
husika.
Zawadi kubwa na ya jumla itatolewa kwenye sanduku la dhahabu, na pia
washindi wote wa mwezi wa sita watapata nafasi ya kuchagua sanduku la dhahabu
wanalolipenda kila mmoja na ndani yake kutakuwa na zawadi mbalimbali
- 2 iPad mbili (2)vocha tano (5) za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya shilingi laki mbili za kitanzania (Ths 200,000) kila moja, mashine za kufulia nguo mbili (2), na cinema moja (1) ya ndani.
- Vocha za manunuzi za Shilingi 200,000 kila moja.
- Mshine za kufulia mbili (2)
- . Shindano hili litafanyika kila wiki ya kwanza ya kila mwezi na kuzingatia walioingia kwenye shindano mwezi uliotangulia.
No comments:
Post a Comment