Afisa Mtendaji Mkuu PepsiCo, Asia, Mashariki ya Kati na Africa Bw.
Saad Abdul-Latif akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa SBC Tanzania Bw. Ziad
El Khalil.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo akifurahia jambo na Bw. Saad Adbul-Latif. |
***** ******
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya vinywaji baridi ya PEPSI kwa Bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw.
Saad Abdul Latif, hivi karibuni alifanya ziara nchini Tanzania ikiwa ni sehemu
ya ziara ya kuzitembelea nchi za ukanda wa Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na
Uganda).
Katika ziara hiyo, Bw. Latif,
aliambatana na Rais wa Kampuni hiyo ya PEPSI kwa bara la Asia, Mashariki ya
Kati na Afrika, Bw. Sanjeev Chadha, ambapo waliweza kukutana na kufanya
mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce
Mapunjo.
“Ni furaha kubwa kuwa hapa
nchini Tanzania. Kubwa ninaomba muwe na uhaikika ya kwamba Kampuni ya PEPSI,
imedhamiria kuhakikisha kwamba wateja wake wanafurahia bidhaa zenye ubora wa
kimataifa katika bei nafuu zilizo za kirafiki,” alisema Bw. Latif.
Akizungumza kwa niaba ya
Serikali, Bi. Mapunjo aliishukuru Kampuni hiyo ya PEPSI kutokana na ahadi yake
iliyojiwekea ya kusaidia katika suala zima la maendeleo ya kiuchumi hasa katika
juhudi zake za kuboresha viwanda, masoko, miundombinu na usambazaji.
“Kampuni ya PEPSI nchini (SBC
Tanzania) inazalisha na kutengeneza nafasi za ajira nchini Tanzania,” aliongeza
Bi. Mapunjo.
Hivi karibuni Kampuni ya SBC imeanzisha
kiwanda cha kisasa cha PEPSI katika jiji la Nairobi, ambapo matokeo yake
yamekuwa mazuri naya kutia moyo kutoka kwa wateja. SBC si tu inatoa chaguo la
ziada kwa wateja wake kwenye vinywaji vyake, lakini pia inatoa thamani ya ziada
kwa fedha.
Vinywaji hivi vya PEPSI venye
ujazo wa 350 ML kwenye glasi kinauzwa bei ya kawaida ambayo ni sawa na bei ya
chupa yenye ujazo wa 300 ML. Ni pamoja na Pepsi, Mirinda, Mountain Dew na aina tofauti
za Evervess Kampuni ya SBC Tanzania, ni kampuni pekee inayozalisha bidhaa
mbalimbali za PEPSI nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment