Mwenjuma Magalu (wa kwanza kulia mstari wa pili) ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha
pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo akiwa darasani na baadhi ya wanafunzi wenzake
alipotembelewa na mwandishi wa habari hizi.
Na Thehabari.com, Handeni
UTAFITI
wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA), Machi 2012 umefanikisha kumrudisha shuleni mwanafunzi
wa sekondari aliyekuwa ametelekezwa yeye pamoja na familia yao.
Mwenjuma
Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya
Sekondari Komnyang’anyo alitelekezwa na babayake yeye pamoja na
mamayake mwaka jana, hivyo kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza
katika shule hiyo licha ya kuchanguliwa kuendelea na masomo.
Hata
hivyo baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya
Handeni na taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na sekondari baada
ya mamayake (kwa sasa marehemu) kukosa uwezo kuripotiwa, alijitokeza
mfadhili wa kumsomesha ambaye anagharamia masomo yake hadi sasa.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni Komnyang’anyo,
mwanafunzi huyo aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa
umma na kupatikana kwa mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya
familia yao kutelekezwa.
“Binafsi
nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi
shuleni…hii kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa
amekata tamaa kabisa kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua
mitaani huku wenzake wakiendelea na shule,” alisema bibi wa mtoto huyo,
Amina Mohamed akizungumza.
Bibi
huyo akizungumzia maisha ya sasa ya familia hiyo alisema bado
wanahitaji msaada wa huduma hasa baada ya mwanaye kufariki dunia mwaka
jana na kumuachia watoto wake.
Aliongeza
kwa sasa yeye ni mgonjwa wa TB anayetumia dawa hivyo kwa hali yake
ameshauriwa kupumzika jambo ambalo limempa mzigo mkubwa kimajukumu
mwanafunzi (Mwenjuma), kufanya kazi za nymbani kama kupika kulima na
shughuli nyingine.
Hata
hivyo mama wa mtoto huyo (Hadija Magalu) ambaye alitelekezwa na mzazi
mwenzake alifariki dunia mwaka jana kwa tatizo la uzazi na kuiacha tena
familia hiyo ya watoto watatu katika hali ngumu zaidi chini ya malezi ya
bibi mzaa mama.
No comments:
Post a Comment