Na Mwandishi Wetu
Uzinduzi wa shindano la kumtafuta Miss Tabata
2013 unafanyika leo Da West Park, Tabata jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, jumla ya walimbwende 26
watambulishwa kwa mashabiki kwenye onyesho hilo ambalo litaenda sambamba na
kusherekea sikukuu ya Pasaka.
Mratibu wa shindano hilo, Joseph Kapinga alisema
jana kuwa warembo hao watatambulishwa pamoja na washiriki wa Miss Mzizima.
Kapinga aliwataja warembo wa Tabata
watakaotambulishwa kuwa ni Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya
David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice
Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21),
Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Aliwataja wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian
Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin
Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19),
Blath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22).
Utambulisho wa warembo hao, utasindikizwa na
burudani kabambe kutoka bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”.
Kapinga alisema wapenzi wa tasnia ya urembo
Jijini Dar es Salaam, watapata fursa ya kuwaona warembo hao leo kabla ya
shindano lenyewe litakalofanyika Mei mwaka huu.
Onyesho hilo limedhaminiwa na Konyagi, CXC
Africa, Fredito Entertainment na Saluti5 na kuandaliwa na Bob Entertainment na
Keen Arts.
Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki
Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela
Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
No comments:
Post a Comment