March 21, 2013

TIMU YA WATANZANIA YAWAONDOA WANA AFRIKA MASHARIKI KATIKA KIPINDI CHA KWANZA KABISA CHA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™



Washindi wa kipindi cha kwanza cha Guinness Football Challenge kilichooneshwa jana katika Televisheni za ITV na Clouds TV Mwalimu Akida Hamad(kushoto) na Daniel Msekwa(kulia) katika picha ya pamoja na waenesha kipindi Flora Tumsiime na Larry Asego jana baada ya kipindi.


Timu zilizoshiriki kipindi cha kwanza cha Guinness Football Challenge kutoka kushoto wenye nyekundu ni timu kutoka Kenya Stephen Githinji na Michael Kirwa, wenye bluu ni Mwalimu Akida na Daniel Msekwa timu kutoka Tanzania, wenye rangi ya kijani ni timu kutoka Uganda  Kennedy Andindu na Oscar Boban na mwsho timu nyeusi pia ni kutoka Kenya Oscar Litonde na Daniel Muthendu.
 *****    ****
 Jana usiku kupitia televisheni  za ITV na Clouds TV za jijini Dar Es Salaam,kwa staili ya  GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™, Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad kutoka Tanzania walioonesha kwamba  hakuna kisichoshindikana na hakuna kufa moyo kabisa katika mchezo huu ambao sasa hivi unatazamwa na wengi barani Afrika.

Wawili hao waliishia kwenye sare kwa raundi mbili na kuthubutu kuingia kwenye nusu fainali  ambapo wana nafasi ya kupandisha kitita chao hadi dola za kimarekani  5,500 (USD 5500) kwenye ukuta wa pesa wa Guinness.

Daniel na Mwalimu walionesha umuhimu wa kutokata tamaa na sasa wameingia kwa kishindo kikubwa kuwakilisha Tanzania kupambana na nchi zingine za Afrika.  Kwenye raundi hii ya kucheza na nchi zingine zilizokuwa kwenye jumuiya ya Afrika mashariki, ikumbukwe kuwa  kuna dola za kimarekani 250,000 ($250,000) za kushindaniwa .

Wiki ijayo tutaweza kuona timu zingine nne kutoka hapa hapa Afrika mashariki zikichuana vikali na kuonesha umahiri wao, Je wataweza kuingia na kuwakilisha  nchi zao kupambana na nchi zingine za Afrika?  Je timu nyingine kutoka Tanzania itaweza kuwapiga chini wakenya na waganda ili tuwe na timu mbili kwenye raundi ya ‘Pan Africa ’?

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE,  ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kuanzia jana kitakua kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV, kwa ITV itakua ni saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  na saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku  Clouds TV.

Usisahau  kuwa na chupa ya bia uipendayo ya  Guinness wakati ukitazama kipindi hiki. 

*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.

No comments:

Post a Comment