Rais
Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli
ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye
Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri, John Joel, akisalimiana na Samuel Sitta, katika Ukumbi wa
Karimjee wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis,
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki
jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa
marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi
29, 2013
Rais
Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza
nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa
marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani
Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Rai
Jakaya Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki
dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya
kuuguaa ghafla wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam
juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye
ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa
marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed
Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye
mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani
Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa
safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment