March 24, 2013

QX PUB NDIO MABINGWA WA KUCHOMA NYAMA ARUSHA






Meneja wa QX,Ally Abdalah(kulia) na Mpishi Mkuu wa Bar hiyo, Emanuel Seneyo(wa pili kushoto) wakionyesha kitita cha shilingi milioni moja baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe Munasa(kushoto) ikiwa ni mabingwa wa  Safari Nyama Choma Mkoa wa Arusha yalifanyika katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.Wa pili kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na  Meneja Mauzo wa Kanda, Kitio Wilderson





Mashabiki wa Bar ya QX ya Arusha wakishangilia na Meneja, Ally Abdalah (wa pili kulia) mara baada ya kutangazwa mabingwa wa Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha yaliyofanyika katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.




Mdau mkubwa wa QX Bar ya Arusha, Chocolate akipata kitu roho inapenda





Hapa ni mwendo wa Nyama Choma tu, Jonson Mshana na wenzake wakijumuika ndani ya banda la QX Bar ya Arusha,ambao ni mabingwa wa  
Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha 2013.


Wzee wa Kitambi noma wakiwa katika hema la Mabingwa wa  
Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha 2013, QX Bar ya jijini humo.




Wanahabari nao walikuwepo uwanjani hapo.

 
 




Wzee wa Kitambi noma wakiwa katika hema la Mabingwa wa  Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha 2013, QX Bar ya jijini humo.

********

Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog Arusha
QX Pub, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa Arusha, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.

Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa General Tyre, baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja pamoja na cheti.

Waliokuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo mkoani hapa, Royal Stop Over Pub, walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha Sh 800,000 na cheti, wakati Blue Line Pub walishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh 600,000 na cheti.

Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya Rombo Delux iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya VIP Longe ilishika nafasi ya tano na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.

Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.

Alivitaja vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa.

Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani hapa kabla ya kuhamia mkoa wa Moshi na wa mwisho.

“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Arusha tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate nyama bora,” alisema.

Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka takriani 36 na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo  ndio inayoongoza kwa mauzo.

Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, NyerembeMunasa, aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.

“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,” alisema.

Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha yale waliyokosea mwaka huu.

1 comment:

  1. Chezea QX WEWE!.....Wazee wa KITAMBI NOMA

    ReplyDelete