Mwenyekiti wa Maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam leo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo lenye kauli
mbiu ya Amani na Upendo. Kulia ni Mdau wa muziki wa Injili, Mcharo Mrutu.
Na Francis Dande
WARATIBU wa tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye Uwanja
wa Taifa, jijiniDar es Salaam hapo Machi 31, wamepanga kutumia sehemu ya
mapato ya kiingiliokujenga kituo cha watoto yatima kama
ishara ya shukrani kwa jamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati
maalumu inayoratibu tamasha hilo
la kimataifa, Alex Msama, alisema kituo hicho kitakachokuwa chini ya kampuni ya
Msama Promotions kitajengwa eneo la Pugu.
Alisema uamuzi huo umefikiwa kwa lengo la kuwapa faraja
watoto yatima ambao nao wana haki ya kupatiwa matunzo na mahitaji muhimu katika
makuzi yao ikiwemo elimu katika kujenga taifa bora la kesho.
“Tangu kuasisiwa kwa tamasha la Pasaka mwaka 2000, tumekuwa
tukirejesha sehemuya mapato ya viingilio kwa jamii kwa njia ya misaada kwa
yatima, wajane na walemavu, lakini safari hii tumeona twende zaidi ya hapo kwa
kujenga kituo cha watoto,” alisema.
Alisema lengo ni kujenga kituo hicho cha kisasa ambapo kama
mipango itakwenda vizuri, kitakamilika kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza
muda wake kwani wangependa ndiye akizindue kwa kutambua mchango wake kwa
tamasha hilo.
“Mwaka 2011, Rais Kikwete ndiye alikuwa mgeni rasmi wa
tamasha letu paleDiamond Jubilee, jijini Dar es Salaam .
“Kitendo cha Rais kuacha kazi nyingi na kuja kutuunga mkono
kwenye shughuli hii ya kiroho, kwetu ni
jambo kubwa sana
ambalo kamwe hatutalisahau, hivyo tumeona tumpe heshima hiyo ya kuzindua kituo
hicho akiwa bado madarakani,” alisisitiza.
Msama ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki
wa injili kujitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za kampuni yake kuandaa
tamasha hilo kwa malengo mbalimbali ikiwemo kueneza injili ya Mungu na kusaidia
makundi maalumu.
Kuhusu waimbaji, Msama alisema wale wa nje wataanza kuwasili
wiki ijayo na kuongeza kuwa hadi kufikia Ijumaa, waimbaji wote watakuwa wamefika tayarikwa tukio hilo
mbalo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Aliongeza kuwa idadi ya waimbaji imeongezeka baada ya kujitokeza
kwa mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Ntutuma kutoka nchini Kenya.
Baada ya kishindo cha tamasha hilo
kutikisa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ,
itakuwa zamu ya Dodoma ,
Iringa, Mbeya, Mwanza kabla ya mashambulizi kuhimishwa mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment