Jengo
lililo pembeni mwa msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi
katikati ya jiji la Dar es salaam linavyoonekana baada ya kuporomoka
asubuhi hii. Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova
kawaambia wanahabari kuwa kila aliyehusika na ujenzi, usimamizi na hata
utoaji vibali atawajibishwa endapo kutaonekana kumekuwepo uzembe upande
wake
**********
Magari yalifukiwa na kuharibika vibaya
Vijana walikuwa wakicheza mpira jirani na jengo hilo nao walijeruhiwa vibaya
Zege kama hili kwa mikono tu bila vifaa vyauhakika ni ngumu kulitoa.
INAELEZWA
KUWA MPAKA SASA WATU 17 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA WAMEPOTEZA
MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA WENGINE WENGI
WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.
MKUU
WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK PAMOJA NA
VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AKISHIRIKIANA
NA WADAU WENGINE WA VYOMBO MBALI MBALI VYA ULINZI NA USALAMA,KUHAKIKISHA
UOKOAJI UNAFANYIKA KWA WAKATI.
AIDHA UHABA WA VIFAA VYA UOKOAJI UNAWEZA KUCHELEWESHA ZOEZI HILO LA UOKOAJI. MINONGONI MWA VIFAA VINAVYOHITAJIKA HAPO NI PAMOJA NA MASHINE ZA KUPASULIA ZEGE, SCAVETA KWAAJILI YA UFUKUAJI.
CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA JENGO HILO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA,KWANI KILA MTU YUPO KWENYE HEKAHEKA ZA UOKOAJI.
PICHA NA VIDEO ZA TULIO HILO LA KUSIKITISHA ZITAWAJIA PUNDE TU,HIVYO TUVUTE SUBIRA KIDOGO. SOURCE: MICHUZI MEDIA
No comments:
Post a Comment