Na
Mwandishi Wetu
JUMLA ya
warembo 23 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013
ambalo litazinduliwa siku ya Pasaka kwenye ukumbi wa Da’ West Park Tabata.
Mratibu wa
shindano hilo, Godfrey Kalinga alisema jana warembo hao watatambulishwa pamoja
na wale wanaoshiriki Miss Mzizima siku ya sikukuu ya Pasaka Da West Park.
Kalinga
aliwataja warembo waliojitokeza kuwania taji la Miss Tabata 2013 na kuendelea
na mazoezi Da West Park ni Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya
David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice
Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21),
Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Aliwataja
wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida
Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19),
Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Blath Chambia (23), Ray Issa (22),
Shamim Abass (22) na Shan Abass (22).
Utambulisho
wa warembo hao, utasindikizwa na burudani kabambe kutoka bendi ya Twanga Pepeta
“Wazee wa Kisigino”.
Kapinga
alisema wapenzi wa tasnia ya urembo Jijini Dar es Salaam, watapata fursa ya
kuwaona warembo kabla ya Miss Tabata kufanyika Mei mwaka huu.
Miss
Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment na
Saluti5 na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
Washindi
watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia
taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
No comments:
Post a Comment