Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akionyesha kipeperushi cha huduma ya SMS kichizi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo itakayowawezesha wateja wa Airtel nchini kutuma ujumbe mfupi wa sms kwa shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde.
*****
Airtel Tanzania kampuni ya simu inayoongoza kwa mtandao mpana na huduma bora na bei nafuu leo imetangaza bei mpya yenye punguzo la gharama za kutuma ujumbe mfupi ili kuwapati wateja wake urahisi na unafuu wa huduma ya ujumbe mfupi nchini. Airtel imepunguza gharama za sms kutoka shilingi 54 hadi shilingi 1 kwa kila sms.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa gharama mpya ya sms Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami alisema” Leo tunayofuraha kuzindua SmS Kichizi ofa ya peeke itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu. hii ni ya kwanza kutoka Airtel ambapo tumewapatia na kuwawezesha wateja wetu nchi nzima kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu ya shilling 1 kwa kila ujumbe mfupi kwenda kwenye mtandao wowote masaa 27 siku 7 za wiki bila kikomo. sasa wateja wa Airtel watatozwa shilling 125 kwa ujumbe wa kwanza wa sms na zingine zitakazofuata zitatozwa gharama ya shilling moja kwa siku”.
“SMS kichizi huduma ya ujumbe mfupi ni mwendelezo wa kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma bora, kuwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu za wateja na kutoza gharama nafuu. Airtel leo ndio mtandao ulioenea zaidi maeneo mengi nchini na kuwafikia watanzania wengi zaidi kupitia huduma zetu za Airtel money na internet yenye kasi zaidi nchini.” aliongeza Ndikumwami
Gharama hizi mpya za ujumbe mfupi zitatozwa kwenda mitandao ya ndani ya nchini tu na ni kwa wateja wa Airtel wa malipo ya awali nchini.
Akiongea kuhusu muda wa huduma hii Francis Ndikumwami alieleza, Airtel tunawajali wateja wetu hivyo huduma hii ya SMS Kichizi sio promosheni ni huduma ya kudumu.
Airtel bado inaendelea na promosheni yake ya msimu wa sikukuu ya Amka millionea ambapo wateja wengi nchini nzima wameendelea kujishindia pesa taslimu ambapo wateja zaidi ya 300 wameshajishindia jumla ya pesa taslimu zaidi ya shilling million 120 hadi sasa.
No comments:
Post a Comment