January 02, 2013

MAMA TUNU PINDA ASHIRIKI MKESHA WA MWAKA MPYA SAMBAMBA NA TAMASHA LA WANAWAKE MKOANI RUKWA (RUKWA WOMEN IN ACTION)

 Pombe ya asili ya kabila la wafipa inayotengenezwa kwa ulezi na kunyewa kwa mirija, raha duniani.
Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika ukumbi wa St. Maurus Chemchem Mjini Sumbawanga jana katika sherehe aliyoalikwa na Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya ya kuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka 2013 iliyoenda sambamba na tamasha kubwa la mwanamke wa Rukwa RUWA (Rukwa Women in Actiion). 

Tamasha hilo lililobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa lina lengo la kuwanunganisha wanawake wa Mkoa wa Rukwa pamoja katika tamaduni zao tofauti katika kuwainua kiuchumi na kifikra ambapo walishiriki kwa kuonyesha tamaduni zao za ngoma, mavazi na chakula. Lengo la tamasha hilo pamoja na umoja huo ni kwa ajili ya kunadi na kuhamasisha utalii wa ndani, kuwawezesha kinamama wa kipato cha chini, kuhamasisha na kuwezesha vita dhidi ya umaskini, mimba za mashuleni, lishe bora na chanjo za afya kwa watoto wachanga na wanawake wa kipato cha juu kuwawezesha wa kipato cha chini.


Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake katika tamasha hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika tamasha hilo kumkaribisha mke wa Waziri kuzungumza na washiriki zaidi ya mia sita walihudhuria katika tamasha hilo.
Mama Pinda (kulia), Mama Dora Rajab Rutengwe mke wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya na wanawake wengine wakijumuika kucheza muziki wa kwaito katika kupasha misuli moto kwenye tamasha hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akionyesha vazi linalotangaza utalii wa ndani na rasilimali muhimu kama misitu, wanyama pori, na samaki.
Ilifika muda washiriki wa maonyesho hayo kupita mbele ya jukwaa kuu tayari kwa kuanza kuonyesha sanaa na mitindo mbalimbali.
Mmoja ya washiriki akionyesha moja ya vazi la kiutamaduni la asili ya makabila ya Rukwa kwa wazee wakati wa msimu wa baridi.
Katibu tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisakata ngoma ya kinyaturu katika tamasha hilo. Kulia ni mwanae Hussein Chima.
Mama Tatu Chima mke wa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akimpa zawadi ya shanga za kabila la kinyaturu Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kabla ya kuanza kucheza ngoma ya kabila hilo. Kulia ni mumewe Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (wa pili kushoto) Injinia Stella Manyanya akishiriki kwenye ngoma ya kabila lake la wangoni waliojumuika kwenye tamasha hilo kuonyesha baadhi ya tamaduni zao. Wa kwanza kushoto akionyesha uwezo mkubwa katika kusakata ngoma hiyo ni mwandishi wa habari wa channel ten Judy Ngonyani.
Mduara pia umo katika ngoma za kabila la wangoni. 

Washiriki wa kabila la wahaya wakionyesha baadhi ya mavazi ya asili ya kabila lao.

Ngoma za kihaya.

Majaji waliohusika katika katika mashindano ya tamaduni za makabila tofauti ya Mkoani Rukwa, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Kagera, Singida, Kigoma, Shinyanga na Mwanza. Mkoa wa Rukwa ulishinda katika Ngoma.
 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha baadhi ya mavazi yao ya asili na baadhi ya zana zao za asili. 

 Sound ya ngoma ya kabila la wafipa ikitumbuiza katika tamasha hilo. Kigoda hutumika kusugua chungu ambacho hutoa mlio wa aina yake katika kunogeza ngoma ya kabila hilo.

 Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha tamaduni zao za kusaga unga na ulezi kwa kutumia zana za asili.
 Mambo yetu ya rusha roho nayo yalikuwepo. 

 Palikuwa hapatoshi.

Mvua ya shampen ya kukarisha mwaka mpya 2013 ikifunguliwa na mratibu wa tamasha hilo ambae pia ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Ndugu Deonisya Njuyui.

 Cheers kwa mwaka 2013. Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu akigonganisha glass na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla na Mke wa aliyekuwa Mbunge jimbo la Sumbawanga Mjini CCM Aeshi Hillal.

 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Idd Kimanta akinywa togwa iliyoandaliwa na kabila la wahaya.

 Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kandege nae akilamba tongwa.

 Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakionja ugali wa muhogo ulioandaliwa na kabila la Waha kutoka Kigoma.
  
 Ndizi kuku au Kuku ndizi kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.

 Maharage yaliyochanganywa na mboga za majani kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.

 Mshiriki Leah Mgagama kutoka katika kabila la wangoni akionysha moja ya vazi la kabila hilo na kifaa cha kuhifadhia chakula kisiharibike kijulikanacho kwa jina la "Kijamanda".

 Vazi la kitanzania likiwa na bandera ya taifa.

 Ilikuwepo mitindo mbalimbali ya mavazi.

 Onyesho la mavazi

 Onyesho ya vazi la mjamzito.

 Anthonia Nkyabonaki kutoka kabila la wahaya akionyesha mtindo wa mavazi. (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa- rukwareview.blogspot.com) NIKUTAKIE MWAKA MPYA (2013) MWEMA WENYE MAFANIKIO TELE.

No comments:

Post a Comment