December 27, 2012

WAKAZI WA SAMARIA NA SHIDA YA MAJI

Tatizo la maji katika vijiji vingi vya Tanzania limezidi kuwa kero na sugu, na kuwafanya wakazi wengi wa vijiji hivyo ama kupata maji mbali au kupata maji ya matumizi yao ya kila siku kama kunywa, kufulia, kupikia na kuogea katika vyanzo ambavyo vinatoa maji ambayo si safi wala salama. 

Pichani ni wakazi wa Kijiji cha Samaria kilichopo Wilayani Arumeru mkoani Arusha wakisafiri umbali mrefu kwenda kutafuta maji wakiwa na Wanyama kazi wao (Punda) ambao huwasaidia kubeba madumu hayo.

Wakazi hao wa Kijiji cha Samaria ambacho kinakaliwa zaidi na jamii ya wafugaji hulazimika kutoka kijijini hapo hadi jirani na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwaajili ya kupta maji safi ya kunywa na kupikia. 

Serikali haina budi kuwasogegezea wakazi hao huduma ya maji safi Kijijini Samaria ili kuwapa fursa wakazi hao kufaidi Matunda ya Uhuru na pia kuwaokolea muda mwingi wanao poteza hasa akina mama na watoto wa kwenda kusaka maji na kushindwa kufanya shughuli nyingine za kijamii katika familia.
 Wasichana wadogo wa jamii za wafugaji kutoka Kijiji cha Samaria wakiswaga punda wao kuelekea eneo lenye maji jirani na Uwanja wa Ndege wa KIA.
Nimisafara mirefu ya Punda kutoka Kijiji cha Samaria huonekana ikiwa imebeba madumu ya maji.

No comments:

Post a Comment