December 10, 2012

UWF yafanya matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangish​a fedha za kuwasomesh​a watoto wa kike waishio katika mazingira magumu

 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,aitwae Vumi akiimba kwa hisia mbele ya wageni waalikwa.
Pichani juu na chini ni wanachama wa UWF wakiwa na mgeni rasmi sambamba na wageni waalikwa wakiwa kwenye matembezi ya hisani ya kilometa tano,yakiwa na lengo ya kuchangisha shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika wanafunzi 50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.Matembezi hayo yalidhaminiwa na taasisi ya Foundation for Civil Society,kampuni ya Clouds Media gROUP,Securix,ITRATECH LTD,Prime Time Promotions,Cool Blue pamoja na Equip Davith Kahwa.
 Wanachama wa UWF (Unity of Women Friends) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza matembezi yao hisani ya kilometa tano kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasomesha watoto wa kike wa shule ya Tandika na Tabata sekondari ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka kwenye familia duni,matembezi hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki huku mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu,Bi.Elizabeth Missokia (wa tatu kutoka kulia)..
 Wanachama wa UWF (Unity of Women Friends) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Tandika na Tabata sekondari
Mgeni rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu,Bi.Elizabeth Missokia akizungumza machache wakati wa hafla fupi ya kuchangisha fedha za kuwasomesha watoto wa kike wa shule ya Tandika na Tabata sekondari ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka kwenye familia duni,Bi Elizabeth kupitia shirika hilo la HakiElimu waliahidi kutoa shilingi milioni tatu ikiwa sehemu ya mchango wao kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Mwenyekiti wa UWF (Unity of Women Friends),Esther Wakati akifafanua madhumuni/lengo la matembezi hayo ya hisani kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wengine,Easther alisema kuwa lengo la matembezi hayo ni kuchangisha shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika wanafunzi 50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.
Mweka hazina wa UWF (Unity of Women Friends),Bi.Mwate Mwadinda akitoa makusanyo yaliyopatikana kwenye matembezi hayo ya hisani ya Kilometa tano,Mwate alisema kuwa hafla yao imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni kumi na laki mbili,hiyo ikiwa ni hatua ya awali ya muendelezo wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka kwenye familia duni
Meneja Mradi wa SOMKI (Somesha Mtoto wa Kike),Bi Jane Magembe akizungumza machache mbele mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi,kuhusiana mradi/mfuko wa SOMKI unatumika kuwasomesha watoto wa kike waishio katika mazingira magumu,Mradi huo uko chini ya UWF.
Baadhi ya wanafunzi wanaosomeshwa na mfuko wa SOMKI,kutoka kulia ni Khadija Hassan Chizenga anaesoma kidato cha nne shule ya Sekomdari Kunduchi Girls High School pamoja na Ummilkhery Abdallah anaesoma kidato cha sita shule ya sekondari Benjamin William Mkapa high school.
 Wanachama wa UWF wakifurahi jambo. 
 Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika ndani ya Police Oficcers Mess,Oysterbay,jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Matembezi yaliendelea.

No comments:

Post a Comment