December 11, 2012

TAMKO LA SKYLIGHT BAND JUU WA WATU WANAOVUNJA AMANI SEHEMU ZA STAREHE

Uongozi wa Skylight Entertainment na Skylight Band, unatoa tamko la kulaani kitendo cha watu wachache waovu wenye tabia ya kuvuruga Amani kwenye sehemu za burudani. 

Tunapenda kuwahikikishia wapenda burudani wa jiji la Dar es Salaam kuwa tutaendelea kutoa burudani mpya na inayokidhi kiu cha muda mrefu cha wapenda burudani katika fani ya muziki wa live.
Aidha tunakemea vitendo vyovyote vya ubabe wa kizamani usio na tija kwa jamii. 

Tunaamini maeneo ya burudani ni kwaajili ya kukutana, kuburudika, kufahamiana, kuondokana msongo wa mawazo unaotokana na maisha ya kila siku na kutengeneza network na watu mbalimbali kijamii, kikazi na kibinafsi.

 Eneo la burudani sio kwaajili ya kuonesha wengine wewe ni nani na una uwezo gani. 

Tunawaomba wana burudani wote tushirikiane pamoja kuwakemea na kuwafichua, kulaani na kuwatenga wote wanaoashiria vitendo vya uvunjifu wa amani. 

Tunaendelea kuimarisha ulinzi na kuwahakikishia burudani kwa kwenda mbele. 
Karibu Thai Village kila ijumaa ujumuike na marafiki na kupata burudani na ladha za kimataifa. Tunawashukuru wapenzi na washabiki wa Skylight kwa kutupokea vizuri ndani ya muda mfupi.
Mungu ibariki Skylight, Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji
Skylight Entertainment.

No comments:

Post a Comment