HABARI
ZIMETUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA KWAMBA MBUNGE WA ZAMANI WA TABORA MJINI
SIRAJU JUMA KABOYONGA (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA GHAFLA SAA NNE USIKU WA
KUAMKIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
KWA
MUJIBU WA TAARIFA KUTOKA NSSF, AMBAKO ALIWAHI KUWA MWENYEKITI WA BODI
YA WAKURUGENZI WA MFUKO HUO WA JAMII, MAREHEMU KABOYONGA ANATARAJIWA
KUZIKWA SIKU YA ALHAMISI NA MSIBA UKO NYUMBANI KWAKE SINZA, JIJINI DAR
ES SALAAM.
MAREHEMU
PIA ALIWAHI KUWA KUWA MENEJA WA KANDA WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA
MASHARIKI (EAST AFRICAN DEVELOPMENT BANK - EADB) KATIKA OFISI ZAKE
JIJINI DAR ES SALAAM.
TUTAENDELEA KUWAPA TAARIFA ZAIDI KADRI ZITAKAVYOTUFIKIA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMIN
No comments:
Post a Comment