December 05, 2012

SHUKRANI YA MSIBA WA BI HALIMA ABDALLAH AMIN


Ni kwa unyenyekevu mkubwa,  familia za Marehemu Mzee Iddi Mtingwa na Alh. Abdallah Amin Abdallah wa Mwanza wanatoa shukrani zao nyingi  na za dhati kwa wote waliotusaidia katika msiba kufuatia kifo cha mama wetu mpendwa, Bi Halima Abdallah Amin aliyefariki dunia tarehe 25 Oktoba 2012 huko Hyderabad, India na hatimaye kuzikwa tarehe 28 Oktoba 2012 jijini Mwanza, Tanzania.



Shukrani za pekee ziende kwa Balozi wa Tanzania High nchini India Amb. John Kijazi, na timu yake akiwamo Dr. Khery Goloka, kwa kujitolea kwa kila hali, timu nzima ya madaktari wa Apollo Hyderabad, Kituo cha Afya cha Aga Khan na Hospitali ya Hindu Union zote za Mwanza, Medi-Ed Clinic na CCBRT waliyotupa msaada wa kimatibabu ili kumsaidia mama yetu kupata tiba bora. Mapenzi ya Mwenyezi Mungu yana nguvu zaidi. Kweli, sisi wote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.



Tunawashukuru wote, katika Menejimenti na Watumishi wa TPSF, Vodacom Tanzania, TTCL, PSPF na Wadhamini wa Msikiti wa Ijumaa, Madrassa ya Kina Mama wa Taufiq, Halmashuri ya jiji la Mwanza na ndugu wote ndani na nje ya Tanzania, kwa msaada na kutufariji katika kipindi hiki vigumu katika maisha yetu. Wema wenu na huruma mliyotuonyesha ni vina maana kubwa sana kwetu.



Kwa vile si rahisi kutaja kila mtu kwa jina, tafadhali pokeeni shukrani zetu za dhati kwa wote ambao kwa njia moja au nyingine mmekuwa na sisi na kutufariji katika kipindi cha kuomboleza. Hii imeonyesha thamani halisi ya familia, marafiki, na wenzake sisi katika maisha yetu.



Inna Lillahi wa inna ilayhi Raji un – Hakika, sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake tutarejea - Quran 2:156

No comments:

Post a Comment