Serikali
imechukua jukumu la kumhudumia msanii na muongozaji wa filamu Sadick
Juma Kilowolo ambaye anatarajia kuondoka wiki ijayo kuelekea India kwa
matibabu.
Katibu wa
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Wilson Makubi, alisema Sajuki
ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
amegundulika kuwa ana tatizo la kufeli kwa figo na kwamba yuko chini ya
uangalizi na uchunguzi zaidi.
Alisema
kutokana na hali hiyo, serikali imejitolea kumsafirisha msanii huyo kwa
gharama zake na kusaidia katika gharama za matibabu akiwa nchini India.
“Sajuki
anatarajiwa kusafiri wiki ijayo baada ya taratibu zote kukamilika, hivyo
sisi kama TAFF tunathibitisha kuwa hali yake bado haijatengemaa kama
ilivyojulikana hapo awali,” alisema Makubi.
Msanii huyo
amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu ambapo mwaka jana
alianza na uvimbe ulioanzia mikononi na baadaye ndani ya mwili kwenye
ini na sehemu tofauti za tumbo.
Msanii huyo
alipelekwa India kwa ajili ya kutibiwa, kisha akarejea nchini baada ya
kupata nafuu, ambapo kwa sasa ameugua tena na anahitaji matibabu ya
haraka ikiwamo upasuaji.
No comments:
Post a Comment