Tamasha hilo litafanyika katika
uwanja wa Kaitaba na baadae katika Ukumbi wa Lina’s siku ya tarehe 9 mwezi huu
ambayo ni siku ya Uhuru wa Tanganyika.
Akizungumzia tamasha hilo Rose amesema
amejiandaa kusherekea Uhuru kwa aina
yake tofauti na watu wengi walivvozoea kwa kuwashirikisha watoto yatima na wale
wanaoishi katika mazingira magumu.
Nimefurahi kupata nafasi ya
kutumbuiza katika tamasha hili la aina yake hasa katika mkoa wa Kagera ambapo itakuwa mara ya kwanza
kuonekana live katika mji wa Bukoba.
Nawaomba wananchi wa Bukoba
kufika kwa wingi katika tamasha hili la kipekee katika ukuonyesha moyo wa
upendo kushirikiana na kusaidia jamii ya watu wengine wasio jiweza.
“nimejiandaa kuwapa nyimbo mpya
ambazo bado hawajawahi kuzisikia,itakuwa mara ya kwanza kuziimba katika tamasha
hili.alisema
Tamasha hilo la Shangwe Kagera
lina lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na
wanaoishi katika maisha magumu.
Wakati huohuo Enock Jonas 'Zunguka' wamewataka wakazi wa Kagera
kukaa sawa kwa ajili ya tamasha hilo na watarajie kupata burudani ya kutosha na
ya kipekee kutoka kwake ambayo
itawajenga roho ya imani, kupendana na kusaidia watu yatima na watoto wanaoishi
katika mazingira magumu ili nao waweze kufaraia maisha.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula
Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta anasema
kuwa matayarisho ya tamasha hilo yanaendelea vizuri kutokana na mwitikio mkubwa
wa watu mbalimbali waliojitokeza kushiriki.
Pia, Mutta anasema bendi ya muziki
ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya wanakwaya wa makanisa mbalimbali, kikundi cha watoto
yatima wamejitokeza pia kutumbuiza.
“Mpaka sasa tumekamilisha sehemu kubwa ya
matayarisho hayo na tayari tiketi zimeanza kuuzwa katika maeneo yote ya mji wa
Bukoba nje ya mji” alisema.
Lengo la Tamasha:
Ni kuhamasisha
jamii kuishi kwa amani,kupendana na kusaidia watu wengine hasa wasiojiweza
kimaisha ili na wao wajione ni sehemu
yao.
Katika kutambua hilo kampuni yetu iliamua kufanya utafiti
mdogo nakugundua changamoto nyingi katika Mkoa wa Kagera, mojawapo ni kuwa
na watoto wengi wanaoishi katika
mazingira magumu. Baada ya kuliona hili, tulitembelea vituo mbalimbali vya
kulelea watoto hao, mojawapo ni Tumaini
Children’s Centre kinachomilikiwa na
Kanisa la Kiinjili la Ki lutheri Tanzania (KKKT).
Kituo hiki kinalea watoto wote bila kujali
kabila,jinsia wala dini zao, kwa sasa
kituo hiki kinahudumia watoto zaidi ya 800, kwa kuwapatia elimu,chakula, malazi
n.k ambapo kwa muda mrefu kimekuwa
kikipata msaada toka Sweden ambao kwa sasa wametangaza kuusitisha kwa maelezo
kuwa jamii ya Watanzania inapaswa kujifunza na kuanza kuhudumia watu wao
wenyewe.
No comments:
Post a Comment