Mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru
kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema
aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah
Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu
atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.
Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais
Kikwete kwa kumsaidia matibabu,alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam
leo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake
mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve
Dada yake Ray C.
No comments:
Post a Comment