Watu
wanne wa Kundi la “lambalamba” wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa
kijifanya wanafichua wachawi katika vijiji mbalimbali katika maeneo ya wilaya
za Chamwino, Kongwa na Mpwapwa. kumbe wanawatapeli wanavijiji kwa lengo la
kujipatia fedha.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna msaidizi wa Jeshi la
Polisi Bw. David Misime amesema uchunguzi wao umebaini kuwa vitu wanavyojifanya
kuvitoa ndani ya nyumba au maduka ya watu, kuwa ni wao wenyewe hutuma wenzao
kuvipandikiza na baadaye hujifanya wamevikuta kwenye nyumba ya mtu
anayetuhumiwa kuwa ni mchawi.
Aliwataja
waliokamatwa wakiwa wanajiandaa kuendesha shughuli za lambalamba katika kijiji
cha Vilundilo Wilayani Kongwa kuwa ni mwanaume mmoja Mkombozi Salehe, na
wanawake watatu ambao ni Hadija Tupa, Joyce Nhembelo na Siwema Kwaeli, ambao
walikuwa ni kwa ajili ya kuwapikia lambalamba hao.
“Wanawake
waengine hutafutwa kwa ajili ya kulala nao jambo ambalo ni hatari kwani mbali
ya kwamba ni kinyume cha sheria na unyanyasaji wa kijinsia pia upo uwezekano
mkubwa wa kuambukizwa magonjwa ikiwepo UKIMWI.” Alisisitiza Bw. David Misime.
Aidha
alitoa wito kwa wananchi kuelewa kuwa wanatapeliwa fedha zao na hao watu
waliobuni mradi wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwani wamejionea
wenyewe kuwa wanachangishwa fedha kabla ya kuwaita na hata wanaodaiwa kuwa wachawi,
hudaiwa kiasi cha fedha.
Kamanda
David Misime alisema kuwa shughuli wanazoendesha kundi hilo la Lamba lamba ni
kinyume cha sheria za nchi na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binanadamu kwa
kuwaita baadhi ya watu kuwa ni wachawi kwa lengo la kujipatia fedha.
Mkuu
huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma alisema Upelelezi zaidi unakamilishwa ili
wafikishwe mahakamani wakati wowote, pamoja na Ufuatiliaji wa lambalamba
wengine waliokimbia pamoja na viongozi vijiji wanaoshirikiana nao unaendelea.
Wakati huo huo Polisi Mkoani
Dodoma inamshikilia kwa mahojiano IDDI S/O RAMADHANI PANDAUYAGA @ NGOSHA,
MSUKUMA, Mkazi wa DODOMA MAKULU baada ya kulalamikiwa na wananchi wengi kwa
kujipatia fedha kwa njia udanganyifu kuwa anawauzia viwanja.
Kamanda
Misime amesema hadi sasa mtu huyo ameshatapeli zaidi ya Tshs. 24,537,000/=
kuanzia mwezi Agosti, 2012. Kwa kuwarubuni watu kuwa viwanja hivyo ametumwa na
wafanyakazi wa CDA kuviuza.
Bw.
David Misime alitoa wito kwa wananchi wasikubali kurubuniwa kuwa wanauziwa
kiwanja na kutoa fedha bila kuthibitisha kiwanja hicho kama kipo na ni halali.
No comments:
Post a Comment