December 05, 2012

MSAADA ZAIDI UNAHITAJIKA KURUDISHA HALI YA BI ARAFA BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Bi Arafa Issa akiwa katika kitanda cha ward namba 20 Sewa Haji-Muhimbili hosp asubuhi ya leo.
 
Bi Arafa Issa mwenye umri wa Miaka 38 mkazi wa Kijiji cha Narung'ombe wilayani Ruangwa ambae anasumbuliwa na Uvimbe baada ya kuumwa Kichwa na baadae kupata kipele kilichosababisha Uvimbe kama anavyoonekana Pichani, alifikishwa katika Hospital ya Muhimbili baada ya Wasamaria wema walioguswa na hali hiyo pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kujitoa kumsaidia kumsafirisha toka Kijijini kwao hadi Muhimbili Hospital.

Baada ya kufikishwa na kupokelewa amelazwa Block la Sewa Haji Ward na 20 NA Baadae alitakiwa kupimwa kipimo cha CT Scan kufuatia kipimo hicho Wauguzi wake waliambiwa kipimo hicho kina tatizo na kuelekezwa kwenda Regency Hospital kupima hali iliyokuwa ngumu kwao kutokana na gharama kubwa kwao ya kumudu kipimo hichoTshs(264,000/-).

Kwa msaada mwingine Wadau walifanikisha kupimwa kwa mgonjwa huyo na kupatiwa majibu ambayo yanaelekeza kufanyiwa Upasuaji..

Asubuhi ya Leo nilifika katika hospital hiyo na kuonana na Bi Arafa ambae analalamika sana kupata maumizi makubwa Kichwa na kudai kuwa toka amepokewa katika hospital hiyo na kulazwa tarehe 20 NOV 2012 hadi leo ajapata dawa ya aina yoyote zaidi ya panadol anazonunua hali inapomzidi.

Nilifanikiwa kuwasiliana na muuguzi aliekuwepo zamu asb na baada ya kupitia file lake alinikabidhi fomu inayoonyesha mgonjwa anatakiwa apime kipimo kinaitwa MRI Brains na kuelekeza sehemu ya kwenda kulipia kipimo hicho...Baada ya kuwasilisha hiyo fomu imeatakiwa Tshs Laki mbili(200,000)Pia itahitajika gharama ya Operesheni ambayo haikutajwa.

Kwa niaba ya Bi Arafa Nawaomba wadau mbalimbali ndugu na jamaa kusaidia hatua inayofuata kumsadia mgonjwa huyo..Yupo hapo Hospital Unaweza kusaidia kwa njia moja au nyingine.

Kwa Mawasiliano zaidi ya mgonjwa huyo wasiliana nami kwa 0716 483532,,,,0787176221 au 0716483532 Abdulaziz Ahmeid wa Lindi Press Club au abdulaziz762@gmail.com

Nawashukuru wote walioguswa kumsaidia Mgonjwa huyo hadi ilipofikia leo,,Ameen
Bi Arafa akiwa na Msamalia mwema anaemsaidia kuhakikisha hali ya Mgonjwa huyo Inaimarika.

No comments:

Post a Comment