MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika Desemba 21
na 22 mwaka huu Kiromo
View Resort Hotel, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkutano
huo unatarajiwa kushirikisha wanachama 100, na pia watakuwepo wadau mbalimbali wa
TASWA wakiwemo waandishi wakongwe wa habari za michezo wambao watapewa nafasi
ya kuzungumza kwenye mkutano huo.
Wanachama
wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama,
Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi
wa habari za michezo kwa ujumla.
Pia
kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo ili wawe
na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo itajadiliwa
kwenye mkutano huo.
Kamati
ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea
kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite
wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na
uelewa wa kutosha suala hilo lipelekwe kama ajenda kamili ya kuanzisha chama
hicho kwenye Mkutano Mkuu.
Nia
yetu ni kuona tunapiga hatua za kimaendeleo na kuwafanya wanachama wetu
wafurahie kujiunga na chama hiki na waweze kupata mikopo ya kuwasaidia katika
masuala mbalimbali.
Tunawaomba
wanachama wote ambao wanatarajia kuhudhuria mkutano huo wathibitishe ushiriki
wao kwa Katibu Mkuu wa TASWA kwa njia ya email: mgosius@yahoo.com au taswatz@yahoo.com. Mwisho wa kuthibitisha
ni Desemba 15, 2012 saa kumi alasiri ili maandalizi mengine yaendelee na uwepo
wao katika mkutano uthaminike.
Wanachama
ambao wanajua hawajalipa ada ni vyema wakafanya hivyo, kwa kuwasiliana na Mhazini Mkuu wa TASWA, vinginevyo
chama kitafanya utaratibu mwingine wa kuhakikisha ada zao zinapatikana siku ya
mkutano.
TASWA
inaendelea na mazungumzo na wadhamini mbalimbali na Jumatatu Desemba 10, 2012 saa
tano asubuhi katika mgahawa wa City Sports Lounge Dar es Salaam itatangaza
mdhamini wa mkutano huo.
Nawasilisha. Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
03/12/2012
No comments:
Post a Comment