Wakati ikiwa zikiwa zimesalia siku mbili kwa wakristo Ulimwenguni kote
kuazimisha siku ya kuzaliwa Bwana na Mwokizi wao YESU KRISTO siku ambayo
hujulikana kama Christmas, wenyeji wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini hasa Mkoani
Kilimkanjaro wanako toka Wachaga na Wapare hii leo walimiminika kwa wingi
katika misafara ya magari madogo binafsi wakielekea mwakao.
Father Kidevu Blogu, iliyokuwa njiani ikitoka Arusha ilishuhudia
misafara hiyo ya magari yaliyojaa wanafamilia hao ikifukuzana kuwahi kupanda
safu za milima ya Pare na Uchagani.
Kasi ya Mwaka huu kuongezeka kwa magari madogo barabarani inadaiwa
kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma hasa kutokana na kero ya usafiri wa mabasi
na ndege.
Askari wa usalama barabarani nao leo hii walikuwa katika mishe mishe
zao kama kawaida kwa magari hayo mengi kusimamishwa na kufanyiwa ukaguzi wa
hapa na pale na mambo mengine kuendelea.
Jambo kubwa na la kumshukuru Mungu ni kuwa Father Kidevu Blog katika
pepesa pepesa ya jicho la kamera yake halikufanikiwa kuona ajali yoyote ya
magari hayo wala mabasi zaidi ya magari kadhaa yaliyokutwa yakiwa yamechemka
kutokana na kwenda umbali mrefu.
Walichemka na kuamua nao kufanya mambo.
Magari yaliendelea na msafara
Mvua kidogo ilinyesha barabarani lakini haikuleta madhara
Ni magari ya kila namna yalikuwepo.
Mambo ya namna hii ilikuwepo sana tu.
No comments:
Post a Comment