Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) anapenda
kuwatangazia watahiniwa wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Sita
mwaka 2013 kuwa, mtihani huo utafanyika mwezi Februari. Mabadiliko ya
mihula yaliyofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yataanza
kutumika na Watahiniwa wa Kidato cha Nne mwaka 2013, ambao watafanya
mtihani wao mwezi Novemba na Watahiniwa wa Kidato cha Sita mwaka 2014
ambao watafanya mtihani wao mwezi Mei.
No comments:
Post a Comment