KONTENA lililosheheni kondomu za kiume kutoka
nchini India imekamatwa na kuzuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam,
baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini
Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es
Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu
hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1 milioni
zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa
taratibu zaidi za kisheria.
“Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba
zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa
huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au
zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika.
SOMA ZAIDI HABARI HII HAPA: MWANANCHI ONLINE
No comments:
Post a Comment