Nahodha wa Mabingwa wa Soka bara
Afrika, Timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’, Christopher Katongo (pichani), anataraji kukiongoza kikosi chaeke kupambana na kikosi
cha Juma Kaseja Taifa Stars Desemba 22, mwaka huu katika nyasi za Uwanja wa
taifa.
Kocha Mkuu wa timu ya Zambia
(Chipolopolo) ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha
wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki
itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa
Miguu cha Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu,
Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa,
Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni Given Singuluma, Hichani
Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua
Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick
Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
No comments:
Post a Comment