December 01, 2012

JK ATUA MKOANI LINDI KATIKA MAADHIMISHO YA UKIMWI LEO

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika uwanja wa ndege wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani Lindi asubuhi hii ambako anahudhuria maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja wa Ilulu mkoani humo, wadau mbaloimbali wanaojihusisha na masuala ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi wamejitokeza na kushiriki katika maonyesho yenye lengo la kuelimisha na kukumbusha juu ya hatari za ugonjwa wa ukimwi na mbinu mbalimbali za kupambana nao Kushoto ni Mama Salma mke wa Ras Jakaya Kikwete na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Ludovick Mwananzila.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni"Tanzania Bila Maambukizi mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi Inawezekana"

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi Mkoani humo katikati ni Mh. William Lukuvi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera na uratibu wa bunge
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Lindi mjini Salum Barwany wakati alipowasili mjini Lindi asubuhi hii kwenye uwanja wa ndege wa Lindi.
Viongozi mbalimbali wakimlaki Rais Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa Lindi mkoani Lindi leo asubuhi hii. SOURCE: FULLSHANGWEBLOG.COM

No comments:

Post a Comment