BENKI
ya Barclays Tanzania (BBT) imetangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Benki
Bora kwa mwaka 2012 hapa Tanzania. Taarifa hiyo ilitolewa jijini London,
Uingereza, Alhamisi ya Novemba 29 mwaka huu wakati wa hafla ya Tuzo za
Benki ya Mwaka zinazoratibiwa na kusimamiwa na gazeti la Financial
Times.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa
BBT, Bwana Kihara Maina alisema: “Lengo letu ifikapo mwaka 2015 ni
kuhakikisha kila mtu anataka kuja kwetu kwa kupitia kauli mbiu ya
‘Kaweke Pesa Benki’ (Go-to-bank). Heshima hii kubwa kwetu imeletwa na
moyo wa kujitoa wa wafanyakazi kwa kuwahudumia vyema wateja wetu na
hivyo kuyarahisisha maisha yao.”
Bw.Maina
aliongeza: “Kwa jumla Tanzania kuna benki 50 na kuchaguliwa kuwa Benki
Bora nchini ni furaha kubwa kwa wanafamiliwa wa Barclays, wateja na
wadau wote. Hii ni kwa kutambua uwekezaji wetu mkubwa tulioufanya katika
biashara ili kutoa huduma bora kwa wateja wetu.
Tunawaahidi Watanzania kuwa tutawekeza zaidi na kutoa huduma za kibenki zinazokubalika duniani.”
Kwa
mujibu wa jarida lifahamikalo kama ‘The Banker Magazine’, Barclays
imeshinda tuzo hiyo ya mwaka kutokana na matumizi ya Teknolojia ya
Mawasiliano kama vile uwekezaji katika mfumo wa kazi (workflow and
imaging systems), kuanzisha huduma za bure za ATM, kuanzisha huduma za
kibenki kwa njia ya mtandao, maendeleo katika biashata ndogo ndogo na za
kati (SMEs) na kuongezeka kwa faida mwaka 2010 na 2011.
No comments:
Post a Comment