November 29, 2012

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Denver Nchini Marekani wafanya ziara za kimasomo Airtel Tanzania

Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Cheikh Sarr akiongea na wanafunzi  wa stashahada ya juu ya biashara toka chuko cha biashara cha Daniels cha chuo kikuu cha Denver cha nchini Marekani wakati wanafunzi hao waliipotembelea Ofisi za Airtel Makao Makuu Jana  katika ziara za mafunzo na kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya biashara, uchumi na kufahamu zaidi kuhusu Kampuni ya Airtel.  hii ni mara ya pili kwa wanafunzi wa chuo hicho kutembelea Ofisi za Airtel Tanzania

Professa wa  Chuo kikuu  cha Denver Dr. Douglas Allen cha nchini Marekani  akimshukuru Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Cheikh Sarr kwa kuwapokea  na kuongea na walimu na wanafunzi wa elimu ya juu wa chuo hicho wakati wa ziara ya kimasomo nchini na kutembelea ofisi za makao makuu ya Airtel yaliyopo Moroco jijini Dar es Saalam. hii ni mara ya pili kwa wanafunzi wa chuo hicho kutembelea Ofisi za Airtel Tanzania
Wanafunzi  na waalimu wa Chuo kikuu  cha Denver kilichopo nchini Marekani   pamoja na Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Cheikh Sarr wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yao katika ofisi za makao makuu ya Airtel zilizopo Morocco jijini Dar es Saalam.

No comments:

Post a Comment