November 20, 2012

ST AUGUSTIN TAWI LA SONGEA WATISHIA KUGOMA

Wanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Cha St Augustin tawi la Songea wakilaum chuo hicho kwa kutotoa ushirikiano kwa wanachuo hao kwa sera yao inayosema kuwa hawashughuliki na mikopo ya wanafunzi.
 
Kwani sera hiyo imepelekea hadi kutaka kuandamana kwa wanachuo hao kutokana na chuo kuchelewesha kutoa matokeo yao na kuyapeleka bodi ya mikopo ikiwa pamoja na majina ili waweze kupata mikopo .

Mmoja wa wanafunzi wa chuoni hapo amedai hadi sasa bado kuna matokeo amabayo hawaja yapata kutokana na mkufunzi ambaye ameyazuia kwa sababu hajalipwa mshahara wake. Vilevile ameshangazwa kwa sela hiyo ya chuo wakati baadhi ya matawi kama Tabora, Bukoba na Mwanza ambapo ni makao makuu ya Chuo wanaushirikiano na wanafunzo wa vyuo vyao pia wameshapata mikopo.

Kutokana na hali hiyo iliwabidi wanafunzi wa mwaka wa pili wachange elfu tano kwa kila mmoja aliwamkabidhi mmoja wa wahusika wa bodi ya mikopo ambaye pia ni mwanafunzi akashughulikie mikopo yao lakini bado iliwawia ngumu kutokana na kucheleweshwa kupelekwa kwa majina na matokeo yao.

Akiendelea kuzungumza mwanafunzi huyo amesma Naye Profesa Donatus Komba mbaye ni mkuu wa chuo aliondoka na majina pamoja na matokeo hayo ya wananchuo wa mwaka wa pili na kuyapeleka bodi ya Mikopo wakati yeye akielekea mwanza katika kikao, lakini pamoja na kupeleka majina na matokeo hayo kapeleka muda umekwenda cha ajabu hadi sasa mambo bado ni bilabila .SOURCE: DEMASHONES BLOG

No comments:

Post a Comment