Baada
ya shirika la ndege la Precision Air kununua ndege yao mpya aina ya ATR
42-600 na kuwa shirika la kwanza Africa na duniani kumiliki na kutumia
ndege aina hiyo, sasa inawapa fursa mashabiki wake katika mtandao wa
facebook na twitter kuwa wa kwanza kuruka na ndege hiyo.
Ndege
hiyo hiyo ya kisasa ambayo uzinduzi wake rasmi umepangwa kufanywa
tarehe 5 ya mwezi December, ina siti 50 na inatarajiwa kufanya safari
zake kati ya Dar es salaam na Kilimanjaro.
Katika
uzinduzi huo Precision Air itatoa zawadi kwa washindi watatu (3) kutoka
katika ukurasa wao wa facebook. Ili kushinda itakubidi utembelee ukura
wao wa facebook (www.facebook.com/Precisionairtz), kwanza bonyeza LIKE
kama bado hujajiunga na ukurasa huo halafu SHARE picha ya ndege hiyo
iliowekwa kwenye ukurasa huo kisha waambie marafiki zako waLIKE na
kuCOMMENT kwenye picha yako ulioSHARE, Watu watatu (3) watakaoongoza kwa
kua na LIKEs na COMMENTs nyingi kwenye picha yao walioShare moja kwa
moja kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Precision Air watakua
washindi.
Hi ndio picha ya shindano unayotakiwa kuSHARE ili kushinde
[ ANGALIZO : Unatakiwa kushare picha moja kwa moja kutoka kwenye facebook page ya Precision Air]
Mshindi
wa kwanza kwa kua na LIKEs na COMMENTs nyingi zaidi atashinda tiket ya
buuure kwenda kokote ambako ndege za Precision Air zinakwenda, pia
atapata fursa ya kuruka na ndege mpya ATR 42-600 na mwisho atahudhuria
sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya.
Mshindi
wa pili atapata fursa ya kuruka na ndege mpya ATR 42-600 na pia
atahudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya. Na mshindi wa tatu
yeye atapata fursa ya kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya.
Kwa maelezo zaidi tembelea kurasa zao za; facebook
No comments:
Post a Comment