VIJANA hii ni nafasi ya pekee kutimiza
ndoto zako katika maishakwani Kinywaji cha Guinness kupitia mashindano yake ya
Guinness Football Challenge (GFC)
yanakupa fursa hiyo ya kujishindia kittita hicho wewe na mwenzako katika timu
yenu.
UNAWEZAJE KUSHIRIKI! Fika viwanja vya Leaders Club
jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Novemba 24, 2012 na tafuta mwenzako ambaye
mtaunda timu ya watu wawili na hakikisheni wote muwe na umri kuanzia miaka 18
na kuendelea huku mmoja wenu akiwa na kipaji cha kumiliki mpira na kufanya nao
mbwembwe za kila namna (Ball Control) hii ni kuanzia na madana dana na mazaga
zaga yake na mwingine awe na ufahamu wa masuala mbalimbali ya Soka.
Hiii ni kuanzia soka la nyumbani hadi
majuu katika ligi za akina nanihii huko Laliga, Bunda Siliga na kwingineko.
JINSIA: Washiriki haijalishi ni jinsia gani, wakike au wakiume ilimradi tu unajua vyema masuala ya kandanda a.k.a kabumbu a.k.a Soka basi waweza kushiriki.
Timu tano za vijana 10 zitachaguliwa
hapo na kukwea Pipa Januari mwakani hadi Nchini Afrika Kusini kqwa gharama za
Guinness na kushiriki mashindano hayo kwanza kwa Nchi za Afrika Mashariki yaani
Kenya, Tanzania na Uganda halafu washindi watakutana na wakali wengine kutoka
Afrika Magharibi nchi za Cameroon, Ghana na Nigeria.
Ukiwa huko sasa mbali na zawadi zingine
kibao lakini Bingo nono la Shilingi za Kitanzania Bilioni 1 na Milioni Mia nne (1,400,000,000)zitanyakuliwa
na timu washuindi.
No comments:
Post a Comment