Shangwe za hapa na pale zilitawala kwenye viwanja vya Kizota.
Mwenyekiti
mpya wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mmoja wa wasanii wa
muziki wa kizazi kipya aitwaye Magida mapema jana kwenye viwanja vya
Kizota,nje kidogo ya Mji wa Dodoma,ambako kulifanyika mkutano mkuu wa
chama hicho Taifa.
Mh.Komba
kama kawa akiwarusha vilivyo wajumbe wa CCM ndani ya ukumbi wa Kizota
jana jioni mara baada ya matokeo ya viongozi wa juu wa chama hicho
kutangazwa rasmi.
Haaa haaaa Wadau nao kitu cha nyama choma kilihusika kama hivi pia.
Wajumbe
wa CCM kutoka sehemu mbalimbali wakipongezana baada ya kazi nzito ya
kuwachagua viongozi wao wa ngazi ya juu wa chama hicho.Pichani kulia
Mzee Asas akisalimiana na DC wa Bagamoyo, Ahmed Kipozi.
Wazir Mkuu,Mh Pinda akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa CCM nje ya viwanja vya Kizota,mapame jana jioni.
Rais
Kikwete akipiga kura ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama cha CCM Bara
mapema jana kwenye ukumbi wa Kizota mjini Dodoma,Kulia kwake ni Mh
Philip Mangula ambaye ndiye Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
Mh
Januari Makamba alipokuwa akisoma salamu mbalimbali zilizokuwa zikitumwa
kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi,kuitakia CCM uchaguzi wao
salama na wenye amani,mapema jana ndani ya ukumbi wa Kizota.
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya Marlow akiwaimbisha wajumbe wa mkutano
mkuu wa ccm-Taifa mapema jana jioni ndani ya ukumbi wa Kizota,mjini
Dodoma.
Mama
lao kutoka TOT,Khadija Kopa akiwarusha vilivyo wajumbe wa mkutano mkuu
wa ccm-Taifa (hawapo pichani) mapema jana jioni ndani ya ukumbi wa
Kizota,mjini Dodoma.
Wajumbe wakifuatia jambo kwa makini.
wajumbe wakibadilishana mawazo.
Wajasiliamali kama kawa
Wadau wa mtandao nao walikuwepo pia.
Nyama choma ilikuwepo,Wajumbe wa CCM alijinoma pia.
Wajumbe wakiangalia picha zao
No comments:
Post a Comment