KATIKA
kuadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, bendi ya muziki wa dansi
ya Fm Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ inatarajiwa kufanya onyesho la aina
yake siku ya Desemba 14 kwenye ukumbi wa Msasani Club.
Mratibu
wa onyesho hilo, Nassib Mahinya alisema kwamba, usiku huo wa aina yake
utaambatana na shamrashamra mbalimbali zilizoandaliwa ili kuwapa raha
mashabiki watakaojitokeza.
Alisema
kupitia usiku huo ambao pia utawakutanisha wasanii wote waliopata
kupitia bendi tangu kuanzishwa kwake, pia bendi hiyo itaopiga nyimbo
zake kuanzia zile zilizotoka kwenye albamu yao ya kwanza hadi
sasa. “Pia kutakuwa na tukio la kukata keki sambamba na kuwapongeza wale
wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine kuifikisha hapo ilipo
bendi hiyo,”alisema
Mahinya
aliongeza kuwa katika kunogesha zaidi usiku huo wasanii na makundi
mbalimbali wanatarajia kusindikiza wakiwemo kundi la Mapacha watatu
pamoja na wasanii wa kundi la Mtanashati Entertauinment wakiwemo Dogo
Janja, PNC na wengineo.
Onyesho
hilo limeandaliwa na Sinai Entertainment na kudhaminiwa na Mabibo Beer
Wine & Spirit, Mama Mbaga Catering, Africa Media Group, Chonapi
General Supplier, Benny Mlokozi Company , Big Solution, Mtanashati
Entertainment, Eliado Point View, Arafa Salon, Friendship Restaurant na
Masters Club.
No comments:
Post a Comment