Balozi wa kinywaji cha Hennessy Cyrile Gautier
Auriol, akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na mikakati yake ya
kufanya mazungumza na wafanya biashara mbali mbali wa hapa nchini.
***
Na Mwandishi wetu
Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier
Auriol, yupo nchini kwa ajili ya shughuli mbali mbali pamoja na kukutana na
wafanyabiashara wa jiji la Dar es Salaam.
Auriol aliwasili jijini juzi na kufanya mazungumza na
wenyeji wake kabla ya kuelezea nia ya safari yake ambayo lengo kubwa ni kutanua
soko la kinywaji hicho maarufu duniani kwa Watanzania nan chi za Afrika
Mashariki.
Alisema kuwa pamoja na kukutana na wafanyabiashara,
pia atakutana na watu wa sekta tofauti, miongoni mwao ni wanamuziki na
wanamitindo. Ziara ya balozi huyo itakuwa ya siku tano.
Alifafanua kuwa ujio wake ni mara ya pili kwa ukanda
wa Afrika Mashariki na ameona kuna mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara na
hasa katika soko la vinywaji vikali.
Alisema kuwa kinywaji cha Hennessy
kwa sasa ndicho kinatamba katika ukanda huu na hivyo kuna haja kwa Watanzania
kuanza kupartavradha kwa ajili ya kujenga mwili na afya bora. Ikiwa na zaidi ya
historia ya miaka 250, Hennessy inatajwa kuwa kinywaji (Cognac) bora zaidi
duniani.
Pia Auriol
atakutana na wapenzi wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu ikiwemo
chakula cha mchana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi ya wanawake
watakaochaguliwa watapata fursa ya kujifunza historia ya kinywaji cha Hennessy
lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji hicho lengo likiwa kuwafundisha
wanawake namna ya kufurahia kinywaji hicho wakiwa majumbani mwao.
Balozi Auriol pia atahudhuria chakula cha jioni na
wafanyabiashara wa hapa nchini katika mgahawa wa Akemi uliopo katika ghorofa la
Diamond Jubilee. Balozi Auriol atatoa elimu kuhusu Hennessy ikifuatiwa na
uonjaji wa kinywaji hicho pamoja na chakula kitakachoandaliwa na mpishi mkuu wa
hotel hiyo.
Ziara ya balozi Auriol inaenda sambamba na juhudi
nyingine za kutangaza kinywaji hicho hapa nchini, mojawapo ikiwa ni kampeni ya
mabango ya ‘Flaunt Your Taste’ yaliyosambaa jiji zima pamoja na ukamilishaji wa
chumba cha Hennessy kilicho katika Club 327, ambacho balozi Auriol atakizindua.
Balozi Auriol atakuwa na kikao maalumu pia na wapenzi
wakubwa wa kinywaji hicho, na pia atawazawadia mialiko maalumu ya kuingia
kwenye klabu ya wapenzi wa kinywaji hicho ya Afrika mashariki.
Pia atatoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu
kutoka katika bar kubwa za jijini. Lengo kuu la mafunzo hayo yatakayofanyika
katika hoteli ya Southern Sun na George & Dragon ni kuwapa wahudumu ujuzi
utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati
wakiburudika na kinywaji cha Hennessy kwenye bar au hotel wanazozipendelea.
No comments:
Post a Comment